Na Heri Shaaban , TimesMajira Online
MBUNGE wa viti Maalum Mkoa wa Dar es salaam Janeth Masaburi, amempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ,kwa kuwekeza miradi mikubwa ya maendeleo katika nchi yetu
Mbunge Janeth Masaburi alisema hayo jimbo la segerea wakati wa ziara yake ya kuangalia miradi ya maendeleo ikiwemo machinjio ya kisasa yaliyopo Vingunguti wilayani Ilala ambapo Serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan imewekeza pesa nyingi katika mradi huo.
“Ziara yangu dhumuni lake kuangalia utekelezaji wa Ilani katika miradi ya maendeleo ya Serikali ,tunamshukuru Rais wetu na kumpongeza ametoa pesa nyingi katika miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo mradi wa machinjio Vingunguti, miradi ya sekta ya afya, sekta ya Elimu, miundombinu ya Barabara “alisema Masaburi.
Mbunge Masaburi alisema kazi kubwa amefanya Rais hivyo mwaka 2025 kura zote zitaenda kwake za mkoa Dar es Salaam kutokana na mambo makubwa aliyofanya katika nchi hii .
Alisema Rais ana mapenzi mema ametoa pesa nyingi kwa ajili ya machinjio ya Vingunguti wilayani Ilala na wasaidizi wake wamefanya kazi kubwa pia tunawapongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Jamary Mrisho Satura na Meya wake wa jiji hilo Omary Kumbilamoto, wamesimama Imara mpaka mwaka 2024 nyama zitasafirishwa kwenda nje ambazo zinazalishwa Tanzania..
Katika hatua nyingine mara baada kufanya ziara kukagua majengo ya machinjio hayo na kupokea changamoto mbalimbali alisema amezipokea na kuzifanyia kazi ,ikiwemo sehemu ya mfumo wa maji taka amewataka uboreshaji zaidi huku akiwataka waongeze usafi kila wakati.
Wakati huo huo aligawa majiko ya gesi bure kwa wanawake Mama Lishe wa Vingunguti na Kisukuru,na kuwataka wanawake kuunga mkono juhudi za Rais kutumia nishati mbadala ya gesi waache kutumia mkaa na uharibifu wa mazingira waache kukata miti ovyo.
Aliwataka Mama lishe wa Vingunguti kujenga tabia ya kutumia gesi watunze pesa kidogo kidogo wanunue gesi wakati wakisubiri mkaa mbadala kwa matumizi.
Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto ambaye ni Diwani wa kata ya Vingunguti alisema machinjio ya kisasa yaliyopo Vingunguti yapo katika hatua za mwisho kukamilika alimshukuru Rais kuelekeza pesa nyingi katika Machinjio hayo mpaka mwezi February 2024 yatakuwa yamekamilika kwa sasa ujenzi wa awamu ya mwisho mara baada kukamilika nyama ya ngombe inayochinjwa katika nchi yetu itaanza kusafirishwa nje,alitumia fursa hiyo kumpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji hilo pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la nyumba NHC kwa jitihada zao.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua