December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Marufuku ufugaji,uvuvi uvuvi kufanyika maeneo ya umwagiliaji

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

TUME ya Taifa ya Umwagiliaji marufuku wananchi kufuga, kuchunga ama kuvua samaki katika maeneo yaliyotengwa rasmi kwenye shughuli za kilimo cha umwagiliaji.

Akizungumza kwenye maonesho ya wakulima. A wafugaji (88) kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma ,Ofisa Sheria Mwandamizi kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Amina Mweta amesema
sheria inakataza kufanya shughuli hizo katika maeneo ambayo yametangazwa kuwa ni sehemu ya kilimo cha umwagiliaji .

“Kwa mujibu wa sheria ya umwagiliaji maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli ya kilimo cha umwagiliaji ,hayapaswi kutumika kwa shughuli nyingine.”amesema Mweta

Aidha amesema , Kifungu cha 52 kimeanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Umwagiliaji ambao utachangiwa na serikali kuu, wadau wa sekta ya umwagiliaji pamoja na vyama vya umwagiliaji.

Amesema sheria hiyo iyo imebainisha kwamba wakulima wa umwagiliaji wanapaswa kuchangia ada ya huduma ya umwagiliaji kwa kila msimu watakaovuna kwa asilimia tano tu ya mapato ambayo wanayapata.

Awali amesema sheria ya Taifa ya Umwagiliaji imetoa majukumu kwa tume kuratibu, kusimamia na kuendeleza sekta ya umwagiliaji nchini.

“Majukumu mengine ya Tume ni kusimamia na kusajili vyama vya wakulima wa umwagiliaji.