Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Dar
TAIFA Stars full mzuka!, unaweza kusema hivyo baada ya kuongezwa hamasa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuipa milioni tano timu hiyo kwa kila goli watakaloshinda dhidi ya timu ya Taifa ya Ethiopia.
Stars itaikaribisha timu ya Taifa ya Ethiopia katika mchezo wa kufuzu michuano
ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), utakaofanyika kesho kwenye Uwanja wa
Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam, saa 1:00 usiku.
Rais Samia ameziunga mkono Yanga, Simba na Azam FC kwa kuzipa, ambapo Yanga ilifanikiwa kunyakua kitita cha sh. milioni 50 katika michuano ya awali ya Klabu Bingwa Afrika, kwa kuitandika Vital’o ya Burundi mabao 10.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa
alisema jana kwamba Rais Samia atatoa milioni tano kwa sharti lile lile la Yanga, Simba na
Azam FC, ambapo ‘mzigo’ huo utatoka baada ya ushindi wa magoli.
Hata hivyo Msigwa alimuomba, Ahmed Ally akumbushie umahiri wake wa kusoma Qur’an, ili iwe hamasa zaidi katika kuelekea kwenye mchezo huo.
Naye Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally aliwaita Watanzania
kwenda kuujaza uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya kuipa nguvu Taifa Stars
kwenye mchezo wake dhidi ya Ethiopia.
Kwa upande wake Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe alisema
kutokana na umahiri wa kocha wa Stars anaamini timu hiyo itafanya vyema.
“Safari hii tunaye mwalimu anayewajua vizuri wachezaji wetu kuliko mwalimu
yeyote yule, lakini pia kiingilio rafiki kabisa, hivyo Watanzania hakuna kubaki
nyumbani tukawape wachezaji wetu hamasa,” alisema Kamwe.
Hata hivyo alisema, Yanga SC, Simba SC na Azam FC ni wanufaika wakubwa wa bao la
Mama, sasa awamu hii na wao lazima watoe fedha kuwapa Wachezaji kama hamasa.
Afisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe aliwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kesho Jumatano kwenye mechi hiyo ya Stars dhidi ya Ethiopia.
Kwa upande wake Kocha Mkuu wa Taifa Stars Hemed Morocco alisema Wachezaji wake
wanaendelea kufanya maandalizi sahihi kuelekea kwenye mechi ya kesho.
More Stories
NIDA yawakumbusha wananchi kuchukua vitambulisho vyao
Dkt.Kafumu:Uteuzi wa Rais Samia umezingatia katiba
Kliniki ya sheria bila malipo yazinduliwa Kilimanjaro