January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mama,mtoto wadaiwa kulawitiwa na kuuwawa kikatili Dodoma

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.

MWANAMKE mmoja mkazi wa Mtaa wa Muungano A kata ya Mkonze Jijini Dodoma aitwaye Mwanvita Mwakibasi (33) amepoteza maisha pamoja na mtoto wake Salma Silvester (13)mwanafunzi darasa la sita shule ya msingi Mkonze,wakazi wa mtaa wa Muungano, kwa kile kinachodaiwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali maeneo ya shingoni na mgongoni na kuingiliwa kinyume na maumbile na watu wasiojulikana.

Akizungumza kwa masikitiko mtoto mkubwa wa marehemu (jina limehifadhiwa) amesema ilipofika muda wa saa 9 usiku mdogo wake alimfata chumbani na kumwambia haamke akamuone mama yao anatokwa na damu kitandani.

“Baada ya hapo nilitoka na kwenda sebleni nikakuta mlango wa chumbani kwa mama ukowazi  nikapita nikaingia ndani ndipo nikachukua simu nikampigia bibi japo mama mkubwa ni jirani yetu ila sikuwa na namba yake ndipo nikampigia ilinaweze kumpigia aje ndipo akampigia na akaja”,amesema.

Amesema baada ya mama yake mdogo kufika na majirani ndipo walipomchukua na mdogo wake hospitali.

Kwa upande wake dada wa marehemu Pendo Mwanvita amesema ilikuwa muda wa saa nane usiku alipigiwa simu na mama yake kutoka Mbeya kuwa aende kumuangalia mdogo wake kavamiwa na majambazi kwa kapigiwa simu na mjukuu wake wa kiume mwenye umri wa miaka 14.

“Huyo hiyo siku alilala na watoto wake wawili kitandani wakike wawili na yeye hasa mdogo aliamka kwenda msalani akamuamsha mama yake, mama nipeleke uani lakini baada ya kuhamka akaona mama yake ametapakaa damu ndipo ikabidi amuamshe kaka yake akatafuta simu ya mama yake hakuiona ilibidi atafute simu ampigie bibi yake aliyeko Mbeya kwani ndiyo namba ya simu aliyoshika kichwani”,amesema.

Amesema alipofika alimkuta Mwanvita amelala ndipo akaita majirani wakampeleka hospitali na kuongeza kuwa hospitali walikwenda na polisi na kurudi nao nyumbani kwaajili ya kufanya uchunguzi wa tukio hilo ndipo wakapata taarifa kuwa tayari mmoja kashafariki japo mwingime yupo katika hali mbaya na kuja kufariki baadae wakati akipatiwa matibabu.

Naye Mwenyekiti wa mtaa huo Yona Wami amesema tukio hilo limewashtua sana kutoka na hali ilivyokuwa kwani hawajazoea kutokea matukio ya aina hiyo katika maeneo yao na wamekuwa wakiyasikia katika sehemu zingine yakitokea tofauti na ilivyo sasa.

“Kwanza nashangaa na nasikitika kwanini imetokea hivi yaani hili tukio limetupa hofu kubwa kwasababu matukio ya namna hii sisi hayajawahi kutokea hapa halafu leo hii watu wawili kwa mpigo hii haikubariki hata kidogo lazima uchunguzi ufanyike juu ya tukio kama hili.

Kaiumu mkuu wa kitengo Cha mawasiliano na uhusiano katika hospitali ya rufaa mkoa wa Dodoma,lazaro Mbise amethibitisha kupokea mwili mmoja wa marehemu pamoja na majeruhi mmoja ambaye ni mtoto ambaye baadae naye alipoteza  maisha wakati akiendelea kupatiwa matibabu.

Jitihada za kulitafuta jeshi la polisi Mkoa wa Dodoma kuthibitisha tukio hilo zinaendelea baada ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo SACP George Katabazi kusema yupo kwenye kikao na atazungumza mara ya baada ya kutoka kikaoni.