Na Allan Vicent, TimesMajira Online, Tabora
WATOTO wawili wa familia moja wameuawa na mama yao wa kambo kwa kunyweshwa sumu aina ya super feed NPK na bens attack 344se inayotumika kuulia wadudu kwenye mazao.
Watoto waliouawa ni Dickson Zakaria (5) na Goodluck Zakaria (4) ambao walikuwa wanaishi na baba yao mzazi na kulelewa na mama wa kambo.
Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Richard Abwao amethibitisha kutokea tukio na kubainisha chanzo cha mauaji hayo kuwa ni ugomvi waliokuwa nao wanandoa hao.
Alibainisha kuwa ugomvi huo ulisababishwa na kutotoa huduma za kifamilia ambapo baada ya kuona mzozo unazidi baba mzazi wa watoto hao Zakaria Dotto aliamua kuondoka na kuacha watoto na mama yao huyo wa kambo.
Kamanda alieleza kuwa mama huyo aliamua kuchukua sumu hiyo iliyokuwemo ndani akaikoroga kwenye kikombe na kuwanywesha watoto hao na yeye mwenyewe akanywa.
Aliongeza kuwa baba wa watoto aliporudi alikuta mke wake huyo akitapika sana na watoto wamelala ambapo aliamua kumpeleka hospitalini bila kujua kilichotokea kwa watoto pia.
Alifafanua kuwa aliporudi nyumbani kwenda kuangalia watoto akakuta wameshafariki, na alipoenda kumuuliza mke wake kuhusu watoto akamjibu kuwa amewanywesha sumu ya kuuliza wadudu.
Kamanda Abwao alibainisha kuwa mtuhumiwa (mama huyo wa kambo) anashikiliwa na polisi na atafikishwa mahakamani muda wowote ili kujibu tuhuma za mauaji zinazomkabili.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi