Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
KATIBU Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Abeida Rashid Aballah amesema mtoto Farhia Omar Mohamed (10) ambaye aliyekuwa anapigwa na mamaake wa kambo huko Bububu, Unguja hali yake inaendelea vizuri.
Ameyasema hayo wakati alipomtembea mtoto huyo katika nyumba ya kulea watoto Mazizini, Unguja Abeida amesema mtoto Farhia atapatiwa haki zake zote za msingi kama sheria ya mtoto inavyoeleza, amefahamisha kwamba sheria ya mtoto sheria Na 2 ya mwaka 2011 imeainisha haki za mtoto ikiwemo haki ya kupata elimu, matibabu, kuishi.
Ameeleza ni wajibu wa Wizara ya Maelendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kusimamia utekelezaji wa sheria hiyo kwa maslah ya taifa.
Aidha, katibu Mkuu Abeida ametoa wito kwa wazazi na walezi kutumia busara zaidi wakati wa kumuadhibu mtoto endapo amefanya kosa, kwani ikumbukwe kwamba mtoto ni wa Serikali hivyo, Serikali haitovumilia kuona mtoto anafanyiwa vitendo vya udhalilishaji wa aina yeyote ikiwemo kupigwa, kunyanyaswa, kutelekezwa.
Mtoto Farhia Omar alichukuliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na kuhifadhiwa katika malezi bora.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua