Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Waziri wa fedha Mwigulu Mchemba, amesema malipo ya fidia ya wananchi wa Kipunguni Kata ya Kipawa Wilayani Ilala yanatarajia kuwatangazia mwezi Agosti na Septemba.
Waziri Mwigulu Mchemba alisema hayo katika mkutano wa wananchi 1865 wa Mtaa wa Kipunguni ambao wanatarajia kulipwa fidia mpya ya see werikali kupisha upanuzi wa uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere .
“Nawapongeza kwa uvumilivu wenu wa zaidi miaka 27 toka mwaka 1997 sasa serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, anawalipa rasmi shilingi 143,968,524,641 zimeshapitishwa tunaomba mtupe muda Julai hii mfumo wa Serikali ukae sawa Agosti na Septemba tutawatangazia tarehe rasmi ” alisema Mwigulu .
Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba alisema robo hii ya kwanza itakapoanza watalipwa Wananchi wote 1865 wasubiri kupokea fedha zao barua ya tathimini imeshafika wizara ya FedhaWaziri Mwigulu alisema sakata la fidia ya Wananchi wa Kipunguni Kata ya Kipawa awali Mbunge wa Jimbo la Segerea alifika Dodoma kufatilia na wawakirishi wake Wananchi 30 katika kikao na kila siku Bungeni alikuwa anapigia kelele kuwapigania Wananchi wake ambao walisimamisha nyumba zao kuziendeleza zaidi ya miaka 27 walipwe fidia serikali sasa imeidhinisha kuwalipa .
“Wananchi wa Jimbo la Segerea mmepata Mbunge makini Bonnah Ladslaus Kamoli, anafanya kazi kubwa ya Utekelezaji wa Ilani naomba muuunge mkono katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo Bonnah Ladslaus Kamoli, Mbunge Makini Bungeni anaheshimika ” alisema
Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli, alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kupatia ufumbuzi wananchi wa Kipunguni ambao walisimama kuendeleza nyumba zao wakisubiri fidia mpya ya Serikali ambayo imepitishwa na serikali sasa hivi wanalipwa.
Mbunge Bonnah aliomba Mamlaka inayohusika mara baada kufanyika malipo ya wananchi wake waonyeshe sehemu zitakazopita Barabara Ili Serikali ijenge barabara za kisasa wananchi watakaobaki wapate huduma za Kijamii na Kipawa miongoni mwa kata zitakazojengwa barabara za kisasa mradi wa kuboresha Miundombinu ya Jiji .
Mkurugenzi wa Uhandisi na Huduma za Ufundi kutoka Mamlaka za Viwanja vya Ndege Tanzania (TCAA) Focus Kadeghe alisema mwaka 2016 Serikali ilitunga sheria ya uthamini na usajili wa wathamini mwaka 2023 Serikali kupitia Ofisi ya Kamishina Msaidizi wa Ardhi ,Wizara ya Nyumba na Maendeleo ya Makazi ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam zoezi la uthamini mpya kwa Wananchi wa mtaa wa kipunguni kutumia sheria mpya ulikamilika .
Mhandisi Focus Kadeghe alisema kwa sasa fidia imeidhinishwa na mthamini Mkuu wa Serikali tangu Juni 21/2023 ambapo jumla ya fidia kiasi cha Shilingi 143,968,524,641 zimeshatengwa kwa ajili ya malipo ya Wananchi 1865.
Diwani wa Kata ya Kipawa Aidan Kwezi, alisema suala la sakata la kuwalipa fidia kipunguni limeanza toka serikali ya awamu ya tatu Mbunge Bonnah akiwa Diwani wa Kipawa sasa hivi Serikali ya awamu ya sita Mbunge Bonnah amepambania mpaka amelitatua amempongeza kwa Juhudi kubwa kuwapambania wakazi wa Kipawa.
Diwani Aidan Kwezi alisema Kata ya Kipawa imepata mafanikio makubwa katika miradi mikubwa ya Maendeleo ikiwemo shilingi Milioni 500 Mbunge Bonnah alizielekeza za Barabara ,Mfuko wa Jimbo ametoa Milioni 38,Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini TARURA shilingi Milioni 14 kilima kimechongwa na fedha zingine za Serikali zimeelekezwa sekta ya Elimu Msingi na Sekondari na sekta ya Afya.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba