Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Mwenyekiti Mstaafu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Theophil Makunga amesema mwandishi wa habari anapopewa nafasi ya kufanya kazi yake kwa uhuru unasaidia kusukuma maendeleo ya nchi na Taifa kwa ujumla.
Makunga ameyasema hayo Oktoba 20 2022,jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalumu ya siku moja kwa wahariri na wanahabari yanayoangazia uchechemuzi wa sheria za vyombo vya habari nchini ambayo yanaratibiwa na jukwaa la wahariri Tanzania (TEF).
“Mwandishi wa habari mahali popote ni muhusika katika maendeleo na siyo kwamba ni mdau katika maendeleo au mpinzani katika maendeleo hivyo unapompa nafasi ya kufanya kazi yake kwa uhuru inamaana inamsaidia kusukuma maendeleo katika nchi” amesema.
Makunga amesema wao kama TEF wanaamini kwamba wanapoelekea kuna mwanga unaonekana mbele wa kuwafanya waandishi wa habari waweze kufanya kazi kwa uhuru ili kuleta maendeleo ya nchi.
Akizungumzia kuhusu vifungu vya sheria ya habari, Makunga amesema wanaendelea na mchakato wa mapendekezo ya wadau kutaka mabadiliko Kwenye baadhi ya vifungu kandamizi kwenye sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016.
“Semina hiyo ni muendelezo wa vikao kati ya jukwaa la Wahariri Tanzania TEF na wadau wa habari katika mchakato wa mapendekezo ya wadau kutaka mabadiliko Kwenye baadhi ya vifungu kandamizi kwenye sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016” amesema.
Makunga amesema watawala wengi duniani wanapenda vyombo vya habari viandike habari za kuwasifia hivyo kunapokua na vyombo hawezi akafanya kazi vizuri”
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba