December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makonda: Ni wakati wa CCM kusikiliza kero si hotuba

Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya

KATIBU wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa, Itikadi,Uenezi na Mafunzo,Paul Makonda amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM)ni chama ambacho kinataka kihangaike na kero za wananchi na sio kutoa hotuba ni wakati wa kushughulikia maisha ya wananchi ambao wanachangamoto mbalimbali zinazowakabili.

Makonda amesema hayo wakati akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara na Wananchi katika viwanja vya Ruanda Nzovwe mkoani hapa  ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake  za mikoa  20 katika kusikiliza kero za wananchi.

“Uwe wakati wa chama kiwe na faraja kwa wananchi na matumaini  ya kuishi na chama hiki kimeshashinda dora hivyo hakuna sababu ya kusubiri uchaguzi kwasababu kina wajibu  wa kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata haki yake”amesema Makonda.

Aidha Makonda amewapa salamu watendaji wa serikali kuwa nyakati zimebadilika kwani wanamchukulia kirahisi Rais Samia kutokana na huruma yake na kusema wanaumiza wananchi na kwamba namna bora ya kumpenda,kumheshimisha ni kuwafanyia kazi wananchi wake wanaompigia kura .

“Bahati nzuri nimekuwa mkuu wa wilaya ,Mkuu wa mkoa ,Bunge la Katiba sio Sana lakini naijua serikali nimewaambia huko nilikokuwa napitia nyakati zimebadilika,nafahamu mnapenda Sana mkisikia Rais anaziara sehemu wote mnajaa hamjawahi kufika hata hayo maeneo mnafika pale na kukagua na watu wenu mliowaweka mikoani na wilayani wanawafahamu kuwa huwa hamfatilii mambo mnaanza kusema mheshimiwa mambo yapo safi lakini mioyoni mwenu mnajua ni wanafiki na hamfanyi kazi za wananchi “amesisitiza Makonda.

Hata hivyo Makonda amesema bahati mbaya hategemei mganga na baba yake hajasoma na hapo alipofika kasoma Sana hivyo hana Sababu ya kujipendeza kwa watu ili awe mwema  na kwamba ni bora kujipendekeza kwa Mungu ili watu wake waone furaha ndani chama cha mapinduzi.

Akielezea zaidi Makonda amesema kuwa haiwezekani watu wamepewa jukumu la kumsaidia Rais Samia harafu wamekaa tu ofisini na Rais Samia hawezi kujua mambo yote unalipwa mshahara wa nini kama ofisi imejaa malalamiko.

“Ndiyo maana siku zote nasema Adui wa CCM sio Chadema ,Act  ,Cuf ,na kwamba Adui wa CCM ni mafisadi majitu mazembe yasiyotanguliza utu,na yamekaa kwenye ofisi za umma najua huko mliko hamnipendi na nimeshasema amenipenda Mungu na Rais Samia na ndo maana kila walikokuwa wakisikia tetesi za uteuzi walitafuta watu na kuwalipa fedha na kutengeneza kesi na kuniharibia ili nionekane na mbaya kwa watu “amesema .

Kwa upande Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya, Patrick Mwalunenge amewataka wananchi kuogopa madalali wa siasa na kuahidi kufanya za wananchi .

Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa (NEC)Ndele Mwaselela amesema kuwa watahakikisha wanainyoosha Mbeya kwani haogopi mtu watafanya kazi.