Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
UJIO rasmi wa Katibu wa NEC ,Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM ,Paul Makonda awashushia nyundo watendaji wote serikali kuwajibika ipasavyo katika nafasi na majukumu yao,kwani Chama hakitasita kuwachukulia hatua.
Pia ametuma salamu kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema,Freeman Mbowe kuwa atapigwa kila kona,akienda angani watamfuta kwa sababu CCM inahoja,uwezo na inatekeleza ipasavyo ilani yake.
Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam,wakati wa mapokezi yake rasmi katika ofisi ndogo ya Chama hicho Lumumba,Makonda alisema Mawaziri,Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchini kufanya kazi na kwamba watakaoshindwa ,yeye hatakuwa tayari kuwa msemaji wa chama ambacho watendaji wake hawawajibiki.
”Kazi ya Chama ni kuwa sikio na kuwasemea wananchi,naomba nitumie fursa hii kwa niaba ya CCm kutuma salamu kwa mawaziri wite,wakuu wa mikoa,mkiwakilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na watendaji wote pale itakapobainika hamjafanya kazi yenu kikamilifu Chama hakitasita kuchukua hatua,”amesema.
Amesema hatoweza kusema uongo hivyo kila kiongozi wa serikali atabeba msalaba wake mwenyewe.”Sijahifadhiwa miaka mitatu na miezi mitatu kusema uongo ,sijateuliwa na CCM kusema uongo na katika kiapo chetu kipo wazi kinasema ”fitina ,Uongo,Uzushi,si sehemu ya CCM ,”amesema na kuongeza
”Chama kimepewa dhamana na wananchi walituamini kwa kuunda serikali hivyo kiongozi yoyote atakayebainika na chama haendani na kasi ya kazi na Chama kikajiridhisha hatutuwafumbua macho,”
“Inajulikana kabisa huwezi kumuona muumini anaingia msikitini na viatu,sasa Kiongozi yoyote atakayezembea,chama kitachukua hatua bila kusubiri kwa sababu ni wajibu wetu kukilinda kukitetea na kukipigania,”amesisitiza.
***Akizungumzia Wapinzani.
Makonda amesema taifa halina vyama vya upinzani,bali Tanzania inawatoa taarifa waliojikusanya katika jina la vyama.”Ukimuona Tundu Lissu anaongea sio chama ni mtu tu anatoa taarifa na wakati mwingine taarifa anayotoa inaweza kuwa chanzo ambacho sio cha kweli au sio ya uhakika kwasababu yeye ni mtoa taarifa hana budi kutoa,”alisema .
Makonda amesema kazi ya CCM ni kupokea taarifa zinazotolewa na watoa taarifa hao na kisha wao wanazishughulikia kwa kuanza na yule aliyetolewa taarifa hiyo,
”Nawahakikishia wanachama na wapenzi wa CCM kuanzia leo,Tanzania haina chama cha upinzani bali kina vyama vya watoa taarifa na sisi kama CCM tuitafanyia kazi taarifa zao kwani ni chachu ya ujenzi sio tu wa demokrasia bali maendeleo ya taifa letu,”amesema na kuongeza
”Kipindi cha nyuma nilimuona Kaka angu Mbowe akifanya ziara kanda ya ziwa ,na mimi nimezaliwa Mwanza nimemuomba Chongolo kwenda nyumbani pia nimemuomba kibali chake kwenda pia kumuona Dkt. Mwinyi na Wabunge wa Bunge letu ili nikutane nao na waniambie wanataka Mwenezi wa namna gani,mimi naweza kuwa mwenezi wa namna yoyote,”amesema.
Amesema nchi ya Tanzania inaRais mwenye ngozi ngumu ambaye anatazama mambo kwa macho ya mbali aliruhusu mikutano ya hadhara ili kukuza na kujenga katika lengo lake la kutimiza 4R.
”Juzi nimemuona Mbowe ,Songwe naomba niagize Mamlaka inayoruhusu vibali kama ni watu wa anga nawaelekeza mpeni Mbowe kibali aruke na Helkopta na kama hana mafuta nimeongea na Rais Samia Suluhu Hassani amchangie na kasema atamchangia na akiruka angani nitamfata ,akienda nchi kavu tutamfata ,akiingia kwenye boti tutamfata na atapigwa kila kona,”amesema.
More Stories
Mawakili Tabora walaani kuziwa kutekeleza majukumu
RC Mrindoko:Ufyekaji wa mahindi Tanganyika si maelekezo ya serikali
Walimu S/ Sekondari Ilala wafundwa juu ya maadili ya wanafunzi