Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa,Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda amewashukuru Baraza la Wazee na Wana CCM wote kwa mchango wao wa maombi ya kumpatia jambo jema ikiwa ni sehemu ya baraka na mafanikio.
Mwenezi Makonda ameyasema hayo leo tarehe 19 Januari, 2023 alipopokelewa katika Ofisi za CCM Wilaya ya Kinondoni.
Akizuzungumza katika Kikao hicho na WanaCCM pamoja na Wazee, Mwenezi Makonda amesema heshima ya CCM inatokana na kutatua kero za Wananchi.
“Heshima ya Chama chetu ni kutatua changamoto za watu, tumepewa nafasi na ridhaa maana yake tunanayo majibu ya changamoto walizonazo Wananchi wetu” Amesema Mwenezi Makonda.
Pia, amewataka Viongozi na Wananchama kwa ujumla kuimarisha chama (CCM) kuanzia ngazi za Matawi na Kata.
Aidha, Mwenezi Makonda amebainisha maadhimisho ya CCM yataanza kufanyiwa sherehe kwenye kila Kata na kusema kuwa Wenyeviti wa Kata, Madiwani ndio wenye majukumu ya kuandaa na kila Jumuiya iwe na siku yake ya maadhimisho na lengo ni kuhakikisha maendeleo yote yaliyofanywa kwenye kata yanasemwa ambapo itakuwa chachu ya kuona uhai wa Chama na Jumuiya zetu za Chama Cha Mapinduzi.
Katika hatua nyingine,
Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni wamemkabidhi zawadi ya T-shirt ya Sare ya CCM yenye jina na cheo chake katika chama ikiwa kama sehemu ya kumbukumbu.
Vilevile, wamempatia Sare za Kombati za CCM, Notebook, Kalamu vyote vikiwa na Jina na nafasi yake ya Uongozi katika Chama atakavyoweza kuendelea kutumia katika majukumu yake ziarani.
More Stories
Sherehe Miaka 61 ya Mapinduzi Zanzibar zafana
Simbachawene:Waombaji wa ajira jiungeni na Mfumo wa Ajira Portal
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050