Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC)- Itikadi na Uenezi Komredi Paul Makonda leo October 26,2023 amekabidhiwa rasmi ofisi na Dkt, Sophia Mjema ambae ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais kwenye masuala Wanawake na Makundi Maalumu ambapo mamia ya Wanachama wa CCM walifurika Ofisi Ndogo za Makao makuu ya CCM Lumumba Dar es salaam kumpokea.
Komredi Makonda akizungumza katika Mapokezi hayo, amewatoa shaka wale wote waliodhani yupo na mpango wa kulipa kisasi kwa wale waliomkosea na badala yake atafanya kazi aliyotumwa na Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan na Chama Cha Mapinduzi.
Aidha Makonda amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan na Kamati Kuu ya Chama hicho kwa Imani na dhamana kubwa waliyompatia kiasi Cha kumpatia nafasi kama hiyo na ameahidi kuifanya vyema kazi waliyomtuma.
Pamoja na hayo Makonda ametumia nafasi hiyo kuwaomba Wana CCM na Wananchi wote kumpatia ushirikiano wa kutosha Ili aweze kuifanya kazi kwa ufanisi huku akiwataka Viongozi wakewemo Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu Wilaya na watendaji kuwatumikia Wananchi kwa kushughulika na Kero na Changamoto za Wananchi.
More Stories
Maandalizi ya mkutano mkuu CCM yapamba moto
Jela miezi sita kwa kuvaa sare za JWTZ
Watolewa hofu uvumi juu ya uwepo wa Teleza