November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makonda akabidhiwa mikoba ndani ya CCM

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

ALIYEWAHI kuwa Mkuu Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameteuliwa
kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, akichukua
nafasi Sophia Mjema aliyeteuliwa kuwa mshauri wa Rais Samia Suluhu
Hassan wa masuala ya wanawake na makundi maalumu.

Taarifa iliyotolewa na CCM jana mwingine aliyeteuliwa na NEC ni Rabia
Abdallah Hamid kuwa Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.

Rabia anachukua nafasi Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye ni Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Makonda aliachia nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 2020
na kwenda kugombea ubunge wa Jimbo la Kigamboni akichuana na Dk
Fautine Ndugulile. Katika mchuano huo wa kura za maoni Dkt. Ndungulile
aliongoza.

Wakati huo huo, Rais Samia Suluhu Hassan, ameendelea kuimarisha safu
ya wasaidizi wake, safari hii akimteua aliyekuwa Katibu wa Halmashauri
Kuu (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema, kuwa mshauri wake.

Uteuzi huo wa Sophia, umekuja siku chache tangu alipoteuliwa aliyekuwa
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Jokate Mwegelo, kuwa Katibu Mkuu wa Umoja
wa Wanawake Tanzania (UWT).

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), chini ya
uongozi wa Rais Samia, ambaye ndye mwenyekiti wa CCM, ndiyo ilimteua
mwanasiasa huyo kijana kushika wadhifa huo nyeti ndani ya CCM.

Pia Kamati hiyo ilimteua, Fakii Raphael Lulandala kuwa Katibu Mkuu wa
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba mkoani Songwe.

Wakati watu ndani na nje ya chama wakitafakari uteuzi huo na siri
iliyojificha nyuma ya pazi, Rais Samia ameteua Mjema kuwa mshauriwa
wake katika masuala ya Wanawake na Makundi Maalumu.

Kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa wa Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC)
ya CCM, Itikadi na Uenezi, Mjema alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shnyanga,
wadhfa ambao aliutumika kwa takribani miezi tisa.

Taarfa ya Kurugenzi ya Mawasiano ya Ikulu iliyosainiwa jana na Zuhura
Yunus, ilieleza kwamba Mjema anateuliwa kushika wadhifa huo mpya na
Rais Samia Suluhu.

Uteuzi huo wa Rais Samia unatafsiriwa kuwa ni kuimarisha safu yake
wakati huu wa kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani na
Uchaguzi Mkuu, mwaka ujao.

Kutokana na uwezo wake kisiasa, Mjema anatajwa kwamba atakuwa msaidizi
mzuri wa masuala ya wanawake na makundi maalum kwa Rais Samia, hasa
kwa kuzingatia kuwa mtaji mkubwa wa kura za CCM kwenye uchaguzi ni
wanawake.

Mjema tayari aliyashajipambanua wazi kumuunga mkono Rais Samia, pale
aliposema kinachofanywa na kiongozi huyo anastahili kuendelea kusalia
madarakani kwa miaka 10.

Japo matamshi hayo ya Mjema yaliibua mjadala, lakini kwa mujinu wa
taratibu na kanuni za CCM sio dhambi mwanachama kujipambana na kuweka
wazi maono yake juu ya utendaji wa kiongozi anayefurahishwa na uongozi
wake.

Mjema aliibuliwa kwenye medani za siasa mwaka 2006, alipoteuliwa na
Rais Jakaya Kikwete kuwa Mkuu wa Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.

Baadaye alihamishiwa wilayani Temeke na baadaye Ilala. Baadaye
aliteuliwa na Rais Samia kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Baada ya
kushkiliwa wadhifa huo kwa miezi tisa ndipo alihamishiwa CCM kushika
wadhifa wa Katibu wa itikadi na Uenzi.