December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makatibu wakuu wakutana kujadili maandalizi ya Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 Zanzibar

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt.John Jingu akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi kilichohusisha Makatibu Wakuu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya sensa ya watu na makazi ya tarehe 23 agosti, 2022, kikao kilifanyika katika ukumbi wa hoteli ya Verde Zanzibar.
Mtakwimu Mkuu Zanzibar Bw. Salum Kassim Ali akizungumza jambo wakati wa kikao hicho, kushoto ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula akichangia hoja wakati wa kikao hicho.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Dkt. Laurean. Ndumbaro akifafanua jambo katika kikao hicho.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Allan Kijazi akizungumza wakati wa kikao hicho.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo Bw. Tixon Nzunda akizungumza wakati wa kikao hicho.
Wajumbe wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi wakifuatilia hoja katika kikao hicho.
Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Greyson Msingwa akieleza jambo wakati wa kikao hicho.
Wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi wakifuatilia kikao hicho.
Meneja TEHEMA Ofisi ya TAKWIMU Bi. Mwanaidi Mahiza akiwasilisha mada wakati wa kikao hicho.