Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj Othman Masoud Othman, jana Aprili 15, alijumuika na watu mbali mbali katika Futari ya pamoja iliyofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idris Abdulwakil Kikwajuni, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.
Futari hio iliyowakutanisha viongozi mbali mbali wa Chama hicho kutoka katika Mikoa Mitatu ya Unguja, iliandaliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Katika nasaha zake kwa wanachama hao Alhaj Othman, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Zanzibar, alisisitiza haja ya kudumisha umoja na mshikamano sambamba na kuwahimiza viongozi, wanachama pamoja na wananchi kwa ujumla kuendeleza utaratibu wa kukutana katika mambo ya kheri ili kujenga na kudumisha mahusiano mema.
More Stories
Serikali ,Washirika wa Maendeleo waweka mkakati utekelezaji Dira ya 2050
Dkt.Mpango aipongeza STAMICO kuwa mfano bora utekelezaji matumizi nishati safi ya kupikia
Wezi wa mapato manispaa Tabora kukiona cha moto