Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, leo Januari 3, 2024 amewasili hapo JNICC (Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere) Jijini Dar es Salaam Tanzania, kwaajili ya Ufunguzi wa Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania, akiwa Mgeni Rasmi.
Mkutano huo wa Siku Mbili, ambao unawajumuisha Mawaziri kutoka Serikali ya Zanzibar, na pia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Viongozi wa Serikali, Vyama vya Siasa, Dini, Wasomi na Wanataaluma, Mabalozi na Wanadiplomasia, Wadau wa Demokrasia, Wastaafu, Wabunge na Wawakilishi, Sekta Binafsi, Asasi za Kiraia, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa, Washirika mbalimbali wa Maendeleo, na Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Huo ni Mkutano Maalum wa Pili ambao unalenga pia kujadili Miswada ya Sheria za Uchaguzi na Mswada wa Sheria za Vyama vya Siasa, ambapo Kaulimbiu yake ni “Toa Maoni Yako Kuimarisha Demokrasia”.
Matukio mbalimbali katika picha
More Stories
Mwinyi: Kuna ongezeko la wawekezaji Zanzibar
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Maofisa Watendaji watakiwa kufanya kazi kwa weledi