Na Khalfan Said, Nyakabimdi
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye Viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Makamu wa Rais ametembelea banda hilo leo wakati wa ufunguzi wa maonesho ya mwaka huu ya Nane Nane yanayofanyika Kitaifa kwenye viwanja hivyo.
Makamu wa Rais amepokewa na Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt. Bernard Kibesse na Meneja Uhusiano na Itifaki BoT, Zalia Mbeo ambapo ametembelea idara mbalimbali za Benki hiyo na kuelezwa jinsi zinavyowahudumia wananchi wanaofika kwenye banda hilo.
Maonesho ya mwaka huu ambayo yamebeba kauli mbiu isemayo; “Kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Chagua Viongozi Bora 2020.”
Lengo hasa la maonesho hayo yanayofanyika kitaifa kwa mara ya tatu mfululizo kwenye viwanja hivyo ni kutoa fursa kwa wakulima, wafugaji, wavuvi na wanaushirika kuona na kujifunza matumizi ya teknolojia bora za kilimo, ufugaji na uvuvi kwa ajili ya kuongeza tija na uhakika wa chakula na kukidhi mahitaji ya viwanda na masoko.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
27 kulipwa kifuta jasho Nkasi
Mwakilishi Mkazi wa UN nchini awasilisha hati