Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Alhaj Othman Masoud Othman, jioni ya Leo Alhamis Agosti 22, 2024 amefika na kutoa, Mkono wa Pole kwa Familia ya Almarhum Sheikh Habibu Ali Kombo, huko Nyumbani kwao Kiembesamaki Magharibi ‘B’ Unguja, kufuatia Kifo cha Marehemu Ukhty Khadija khamis Juma ‘Bi Mwalimu’.
Marehemu Bi. Khadija ambaye alikuwa Mwalimu wa Madrasa na Mke wa Almarhum Sheikh Habib Ali Kombo, alifariki-dunia mapema Jana Agosti 21, huko Nyumbani kwake Kiembesamaki, baada ya kuugua kwa muda mrefu; akasaliwa katika Msikiti wa Jamiu – Zinjibar na kuzikwa hiyo hiyo Jana, katika Makaburi ya Michungwani-Milimani, pia katika Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.
Katika ‘Tah-zia’ hiyo, Mheshimiwa Othman ameambatana na Mke wake, Mama Zainab Kombo Shaib.
Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi, Amiin!
Innalillahi Waina Ilayhi Raajiun!
More Stories
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito