January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar aungana na viongozi wengine kuaga mwili wa Hayati Mwinyi

Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline, Zanzibar

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman, leo Jumamosi Machi 02, 2024, amejumuika pamoja na Viongozi wa Serikali, Dini na Wanasiasa Mashuhuri, Viongozi Wastaafu, Mabalozi na Wanadiplomasia, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Familia na Wananchi, katika Hafla ya Kuuagaa Mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marehemu Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya New Amaan Complex Wilaya ya Mjini Unguja.

Mara baada ya hafla hiyo, Othman amehudhuria katika Ibada ya Sala ya Maiti iliyosaliwa hapo Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini, pia Mkoa wa Mjini Magharib Unguja, kabla ya Shughuli ya Maziko yaliyofanyika Kijiji cha Mangapwani Bumbwini, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Katika hafla hiyo ambayo imeongozwa na Mgeni Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Samia Suluhu Hassan, Mheshimiwa Othman ameambatana na Mke wake, Mama Zainab Kombo Shaib.