December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar ashiriki dua maalum yakumuombea marehemu Najma

Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Zanzibar

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Alhaj Othman Masoud Othman, leo Aprili 14, 2024 amejumuika pamoja na Waumini wa Kiislamu, katika Khitma (Dua Maalum) ya Kumuombea Marehemu Najma Khalfan Juma, ambaye aliwahi kushika Nafasi mbali mbali za Uongozi, ikiwemo ya Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia Nafasi za Wanawake,  huko  Kijichi Bububu, kisiwani Unguja.

Katika Dua hiyo, ambayo imefanyika hapo “Masjid Rahman”, Msikiti uliopo Bububu Kijichi Wilaya ya Magharib ‘A’ Mkoa wa Mjini- Magharibi Unguja, Viongozi  mbali mbali wa Kisiasa, Serikali, Dini na Jamii wamehudhuria, wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Dkt. Omar Dadi Shajak.

Kabla ya Ibada hiyo, Mheshimiwa Othman amefika  Nyumbani kwa Marehemu, kwaajili ya kuwasalim Wafiwa, na kuwapa Mkono wa Pole , Ndugu, Jamaa na Marafiki.

Najma, ambaye aliwahi kushika Nafasi mbali mbali za Uongozi, ikiwemo ya Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia Nafasi za Wanawake, alifariki-dunia Aprili 12 katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi- Mmoja, Mjini Unguja alipokuwa akipatiwa matibabu, na kuzikwa Jioni ya Siku hiyo katika Makaburi ya hapo hapo Kijichi, pia katika Mkoa wa Mjini- Magharibi Unguja.