December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar ajumuika katika Ibada ya Sala ya Ijumaa

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Alhaj Othman Masoud Othman, leo Januari 27, 2023 amejumuika na Waumini mbali mbali wa Kiislamu, katika Ibada ya Sala ya Ijumaa, iliyofanyika Masjid Taqwa, Msikiti uliopo Muembe Makumbi-Soda, Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.

Kabla ya Ibada hiyo, Alhaj Othman ametoa Mkono wa Pole kwa Familia ya Almarhum Sheikh Ngwali Ussi (Msaidizi Imamu Masjid Maghfira) Msikiti wa Mchangani Mjini Unguja, kufuatia kifo cha Mzee wao huyo kilichotokea hivi karibuni, ambapo baadae alifika huko Bububu-Kijichi, pia katika Mkoa huo, kumjulia hali Mwakilishi Mstaafu na Mtangazaji Mkongwe, Hajjat Najma Khalfan na Mume wake Bw. Saleh Zam ambao hali zao za afya zilizorota kwa kitambo.