December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makamu Mwenyekiti wa TAMIDA ametembelea banda la Tanzania Expo 2020 Dubai

Na Mwandishi wetu TimesMajira Updates

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA) Osman AbdulSattar Tharia ametembelea banda la Tanzania kwenye maonesho ya Expo 2020 Dubai ambapo amepolekewa na Mkurugenzi wa Banda la Tanzania Getrude Ng’weshemi kutoka TanTrade pamoja na wawakilishi wa Sekta mbalimbali zinazoshiriki kwenye maonesho haya.

Osman amefurahi kuona Tanzania imeshiriki miongoni mwa nchi 192 ikiwa na banda lake linalovutia kwa kuonesha jinsi sekta kadhaa zimeonesha rasilimali mbalimbali zilizopo nchini.

Amesema,” Kwa upande wa Sekta ya Madini, mmeitumia vizuri fursa hii kuonesha ‘Tanzanite’ kwani ni moja ya madini adimu na yenye thamani ulimwenguni. Naunga mkono ushiriki huu na ujio wangu hapa leo utaenda kuongeza msukumo nyumbani wa kuendelea kuhamashisha ushiriki wa uhakika na wenye tija hasa ushiriki katika Wiki ya Madini iliyopangwa kufanyika tarehe 22 Desemba, 2021 mpaka tarehe 4 Januari, 2022 ambapo wadau wote wa Madini wa fursa ya kuja Dubai kushiriki kwenye programu zilizoandaliwa. Nafasi hii tuliyopata tuitumie kikamilifu kuitangaza nchi yetu na rasilimali zitakazofungua fursa mbalimbali ulimwenguni”.