January 30, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makalla :Tuwakatae wanasiasa wachonganishi

Na Agnes Alcardo,TimesmajiraOnline

WATANZANIA wametakiwa kuachana na viongozi wachonganishi kwani wanaleta chuki na uhasama kwenye Taifa na kutozungumzia mazuri yanayofanywa na Serikali.

Hayo yamesemwa na katibu wa NEC Itikadi ,Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Amos Makalla wakati akizungumza na Wananchi na wanachama katika Viwanja vya Umoja ni nguvu kusini Pemba, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake Visiwani Zanzibar.

“Sisi CCM tutatembea kifua mbele kwa kazi ya kuwahudumia wananchi, wale wenzetu ni watu wa vituko, uongo, fitna na majungu ndiyo kazi yao sisi tunajukumu na dhamana ya kuwaletea wananchi maendeleo.

“Nasema hivi kwasababu wanakuja hapa wanasema mnajenga maghorofa wakati watu wanakufa na njaa na miradi yote siyo maendeleo, sasa ndo ujue kuna shida na anaetamka hayo ni mtu mzima ndo mana nasema kazi ni kusema uongo na vituko.

Lakini viongozi hao hao ndugu zao wanasoma katika hayo maghorofa na wanapata huduma mbalimbali lakini hawazioni niseme muda wa kudanganyana umeisha”, amesema Makalla.

Pia Mwenezi Makalla ameendelea kusema kuwa, Dkt Samia Suluhu Hassan na Dkt Hussein Mwinyi hawana ubaguzi wowote kwenye suala la kuwaletea maendeleo wananchi lakini bado kuna viongozi wanasema mabaya badala ya kuyaongelea mazuri yanayofanywa na Serikali hizo mbili.