
Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online Dar.
KATIBU wa NEC, Siasa, itikadi, Uenezi na mafunzo CCM Taifa, CPA Amos Makalla, anatarajia kuanza ziara ya kichama ya siku Saba, kesho Julai 6, 2024 katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi yake, inaeleza kuwa, CPA Makalla, ataanza ziara hiyo kwa kufanya mkutano wa ndani na viongozi wa ngazi zote, utakao fanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee mkoani humo, ambapo pia, atatambulishwa rasmi kuwa Mlezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Dar es Salaam, ikiwa ni muda mfupi baada ya kuteuliwa na Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wiki iliyopita katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC.
Katika muendelezo wa ziara hiyo, CPA Makalla, kwa siku tofauti atapata nafasi ya kutembelea na kufanya mikutano katika maeneo mbalimbali katika Wilaya ya Ilala, Ubungo na Kinondoni.
More Stories
Waziri Mavunde azindua rasmi shughuli za uchimbaji madini Porcupine North -Chunya Mbeya
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Baraza la Taifa la Ujenzi waingia makubaliano ya mashirikiano sekta ya ujenzi
Nderiananga aongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa tatu wa Kimataifa wa watu wenye ulemavu ujerumani