*Juhudi zake zaleta matokeo chanya, watoto wafuatwa nyumbani kupatiwa elimu, aombwa gharama za Oksijeni zibebwe na Serikali
Na Penina Malundo
JUZI (Februali 28, mwaka huu) Tanzania iliungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Magonjwa Adini ili kujenga kujenga uelewa miongoni mwa jamii kuhusu magonjwa yanayotokea kwa kundi dogo la watu hususani watoto.Msukumo wa kupambana na Magonjwa Adimu miongoni mwa Watanzania unatokana na ahadi iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan, alipohutubia Taifa siku alipoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Machi 21, mwaka 2021 akisema;
“Serikali itaweka mipango maalum ya kuhudumia makundi yenye Magonjwa Adimu kwa Watanzania.
” Tangu alipotoa ahadi hiyo, Serikali yake iliweka mikakati yake ya kuhakikisha inasimamia kikamilifu mikakati ya kupambana na magonjwa hayo.Tangu atoe ahadi hiyo tumeona mabadiliko makubwa sana kwenye sekta ya afya na huduma kwa watoto wenye magonjwa hayo, japo safari bado ni ndefu.Leo hii ambapo Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia inaelekea kutimiza miaka miwili tangu iingie madarakani, ifikapo Machi 21, mwaka huu, Serikali ya Rais Samia imeweka mazingira sahihi ya kisera kuhakikisha watoto wenye Magonjwa Adimu wanapatiwa haki sawa na kutoachwa nyumwa katika kuhudumiwa.
Msukumo huo wa Rais umeleta matokeo chanya katika vita dhidi ya magonjwa hayo ikiwa ni pamoja na kuiwezesha Tanzania kujumuika na mataifa mengine kuadhimisha siku ya Magonjwa Adimu duniani.
Aidha, kitendo cha Rais Samia kuweka kwenye vipaumbele vyake magonjwa hayo, kumewezesha Watanzania wengi kuanza kuwa na mwamko na kuyafahamu.Siku ya magonjwa hayo inaadhimishwa kwa kutambua kwamba kuna changamoto nyingi za kidini,kihisia,kiuchumi na kijamii katika kutambua magonjwa haya kwa watu wanaoishi nayo.
Kwa kutambua hilo, dunia iliamua kutenga siku maalum kwa ajili ya kuadhimisha siku hiyo ili kujenga uelewa wa ugonjwa huo ndani ya jamii.
Kwa hiyo kupitia maadhimisho hayo jamii inapaswa kutambua na kuthamini umuhimu wa afya ya watoto wanaoteseka kutokana na magonjwa adimu,sehemu mbalimbali za duniani.
Takwimu zinaonesha kwamba asilimia 72 ya magonjwa haya yanatokana na vinasaba na zaidi ya asilimia 70 yanawakumba watoto wadogo,ambapo takribani magonjwa adimu 7000 yanayojulikana hadi sasa na uathiri ubongo,damu na maini .
Ni magonjwa yasiyopewa kipaumbele cha pekee na jamii husika kutokana na ufahamu mdogo, ukosefu wa tafiti makini kutokana na ukata wa rasilimali fedha na vifaa tiba. Ni ukweli usiopinga Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia imeweza kujitahidi kwa kiasi kikubwa kuhakikisha inaimarisha mipango yake na kuwasogezea huduma mbalimbali kwa watoto waishio na Magonjwa Adimu.Miongoni mwa maeneo ambayo wameboresha ni pamoja katika sekta ya elimu kwa kuhakikisha watoto hao wanafatwa majumbani na kupatiwa elimu.
Sharifa Mbarak, Mama mwenye mtoto aishie na Magonjwa Adimu anasema licha Serikali kuendelea kuweka mipango mizuri kwa watoto hao, wanapata huduma bora lakini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali.
Anasema asilimia kubwa watoto hao wanapoumwa wanaingia katika gharama kubwa kutokana na matibabu yao kutolewa kwenye hospitali kubwa na sio ngazi ya zahanati kutokana na zahanati hizo kutokuwa na vifaa tiba kwa ajili yao. Sharifa anasema watoto hao utakiwa kutumia mashine za kupumulia na kuongezewa Oksijeni muda wote kwa baadhi yao ambapo upatikanaji wa oksijeni ngazi ya zahanati ni wa shida.
Anasema wananchi wengi wanaishi vijijini ambapo huduma nyingi wanazitegemea kutoka kwenye zahanati, hivyo mgonjwa wa ugonjwa huo hawezi kupata huduma ya oksijeni katika ngazi ya zahanati. Akitolea mfano yeye kwa mwanae, Ally Kimara anasema mwanae utumia mashine au kuongezewa oksjeni muda wote na anapotumia mashine gharama yake inakuwa sh. 50,000 ambapo hutumika si chini ya siku tatu.
“Nikisema leo tuongeze Oksijeni ambapo kwa mitungi ya lita 15 ukitumia miwili kwa masaa 24 unajazizwa kwa sh. 80,000 ina maana kila mtungi mmoja 40,000 kwa hiyo utaona ni namna gani gharama inakuwa kubwa kwa wagonjwa hawa,”anasema na kuongeza;
“Katika kuadhimisha siku hii ya watu waishio na magonjwa haya adimu,tunaomba Serikali iangalie haya tunayopitia katika sekta ya afya, kwani sidhani kama kwa maisha yetu Watanzania kwa kipato chetu tunachokipa kama kinaweza kumudu hivi.
Hii hi kwa sababu wazazi wenye watoto hawa wanapunguza au wanaacha kabisa kufanya kazi ili waweze kuwahudumia watoto na hii inafanya kipato chao cha kawaida kinazidi kushuka na kushindwa kuwahudumia,”anasema
.Anasisitiza kuwa hakuna mtu anayelipia pumzi bali watu wote wanapumua pumzi zilizobarikiwa na Mungu ,wito kwa Serikali kuwaangalia watoto hao ambao ni wachache wanaotumia Oksijeni ya ziada ili waweze kupumua maisha yao yote.”Tungeomba Serikali ihakikisha tunapatiwa huduma ya Oksijeni bure au kwa gharama nafuu kwa kila mzazi au mlezi mwenye mtoto wa ugonjwa huo,” anasema na kuongeza:
“Tunaishukuru Serikali kupitia Rais wetu Samia kwa jitihada zake kwa watoto hawa na tumeona tangu alipokuwa Makamu wa Rais hadi alipokuja kuwa Rais alivyokuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha anawawekea mazingira mazuri kwa watoto hawa,”
*** Kuhusu uelewa wa magonjwa hayo adimu Sharifa anasema tangu mwaka 2021 walipofanya maadhimisho ya kwanza nchini Tanzania ya siku ya magonjwa adimu na msukumu uliowekwa na Rais Samia wanaona uelewa ndani ya jamii umeanza kuongezeka ikilinganishwa na kipindi cha kabla ya hapo.Anasema Rais Samia amechochea jamii kuelewa ugonjwa huo pamoja na kuhakikisha watoto wenye ugonjwa huo wanapatiwa elimu na tena kwa kufuatwa majumbani na kufundisha.
“Tunamshukuru sana Rais Samia kwa hili, sasa hivi Ally (mwanae) anakuja kufundishwa na mwalimu wake hapa nyumbani ambaye ameletewa na Serikali na alifanya matihani wake wa darasa la nne na matokeo yake ni mazuri amepata alama A, kwa hiyo naomba na watoto wengine wote nao wapate neema hii na haki yao ya msingi,” anasema na kuongeza;”Pia tunashukuru Wizara ya Elimu kupitia Foundation yetu ya Ally Kimara Rase Disease kwa kufanya mikakati jumuisha kwa hawa watoto kwa kuwapatiwa elimu,na sasa hivi wanaandaa muongozo ambao utajumuisha hawa watoto,tunaona upatikanaji wa elimu sio kama zamani hadi ufike darasani ndiyo upate elimu, sasa hivi hata nyumbani wanafuatwa.”Anasema katika bajeti ya mwaka 2021/22 ya Wizara ya Afya,kundi la watoto waishio na magonjwa adimu iliwataja na kuangizwa kutegwa bajeti ya kuwahudumia wagonjwa hao na wanaona namna huduma inavyowafikia moja kwa moja wagonjwa hao.
”Tunategemea lile fungu likizingatiwa kwa kiwango fulani hata kuelekezwa katika bima ya afya kwa sababu cha msingi ni afya zao, kwani wagonjwa hawa wanajulikana kupitia madaktari wao waweze kuwahudumiwa bila kikomo wala kujali hospitali gani,”anasema.
*** Jamii inachukuliaje wagonjwa hawaSharifa anasema uelewa kwa jamii mwanzo ulikuwa chini ukilinganisha na sasa, kwani hata walipoadhimisha siku ya magonjwa adimu kwa mara ya kwanza watu wengi hawakuwa na uelewa.
Anasema baada ya kutoa uelewa kwa jamii kupitia vyombo mbalimbali vya habari,wachezaji mpira kwa sasa magonjwa haya watu wameanza kuyafahamu.”Ila kwa upana wake elimu kwa umma bado haijafikia moja kwa moja kwa sababu ,tukisema kitaifa ni lazima ifike hadi kijijini,imani za kishirikina kwa watu bado zipo,”anasema.
***Daktari anazungumziaje magonjwa adimu. Daktari Bingwa wa Watoto na Mkuu wa Idara ya Watoto Hospital ya Aghakhan nchini,Dkt.Mariam Noorani anasema magonjwa adimu ni magonjwa ambayo yanatokea kwa nadra hasa kwa wagonjwa wachache duniani.Anasema magonjwa haya utokea kwa watu wachache ni ngumu kuyatambua na kuyafahamu katika jamii na kupelekea hata familia zinazoishi na wagonjwa hawa kushindwa kutambua kwa urahisi magonjwa hayo adimu.
“Kutokana na magonjwa haya kuwa magumu kutambulika imefanya sasa madaktari kuyachanganya na kuwa kundi moja linalotambulika kuwa ni magonjwa adimu na imesababisha madaktari kupata changamoto ya kuyatambua ,kuyatibu,kuyaelezea kwa jamii kwenye lunga itakayoeleweka,”anasema na kuongeza; “Tunaadhimisha hii siku ya magonjwa adimu ili kupaza sauti kwa wataalamu wengine wa Afya, Serikali na Jamii ili wafahamu kwamba haya ni magonjwa yapo.Licha ya kuwepo kwa changamoto lakini mengi yao yanatibika na yale ambayo hayana tiba tunajaribu kuyasema ambapo tunaweza kuishi na mtoto aweze kuishi vizuri,”anasema .Anasema bado kuna changamoto ya vipimo na madawa yanayohitajika hayapatikani hapa nchini hivyo kufanya gharama kuwa kubwa sana katika kuwahudumia watoto hao.
Anasema atashukuru kama Serikali itaendelea kusaidia na kuhamasisha gharama kupunguza kwa wagonjwa hao, kwani wanatumia matibabu kwa gharama za juu ikiwemo masuala ya kuongezewa oksjeni ambayo yanagharama kubwa.***Mahudhurio hospitali Anasema kwa siku za hivi karibuni watoto wenye magonjwa adimu wamekuwa wanaenda katika hospital tofauti na zamani walikuwa wanawafungia kutokana na kutokuwa na uelewa juu ya magonjwa hayo.”Katika jamii kwamba mtoto ni mgonjwa tumpeleke hospitalwatoto hawa wengi wao wanapumulia kwa kufuata oxgeni na mashine za nyumbani na oksjeni zinagharama kubwa na mfumo wa kumtibu mtoto myumbani ni mikubwa na kufanya watoto kukaa muda mrefu miezi hospitali,”anasema
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja