November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Majanga ya moto na dharura yapata mwarobaini

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Ubalozi wa Uingereza na Taasisi ya Mercy Coprps Pamoja na Chuo kikuu cha Dar es salaam kimetoa mafunzo ya namna gani ya kukabiliana na majanga mbalimbali yanayotokea katika jamii na namna ya kukabilina nayo majanga hayo ikiwa ni Pamoja na mawasiliano Pale dharura inapotokea.

Akitoa maelezo Juu ya namna ya kukabiliana na majanga hayo Mratibu wa shirika la Mercy Corps Nchini Bw. Anthony Sarota amesema wameamua kutoa mafunzo hayo kwa Jeshi la Polisi ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na kiteknolojia hasa kwa upande wa mawasiliano Pale majanga yanapotokea.

kwa upande wake kamishna msaidizi wa Polisi ACP Thabitha Makaranga ambaye Pia ni mratibu wa mafunzo hayo kwa upande wa Jeshi la Polisi, amesema Jeshi la Polisi linashukuru wawezeshaji wa mafunzo hayo na kusema kuwa mafunzo hayo yataleta tija na ufanisi kwa Jeshi la Polisi katika kukabiliana na majanga ya dharura pindi yanapo tokea.

Akiongea katika hafla ya kufunga mafunzo hayo leo October 14 Kamishina wa Polisi CP Shabani Hiki ambayo yaliyofanyika jijini Dar es salaam kuanzia October 10 hadi 14 mwaka huu chini ya ufadhili wa ubalozi wa uingereza, taasisi ya mercy corps pamoja na wawezeshaji kutoka chuo kikuu dar es salaam.

AIdha kamishna wa Polisi CP Shabani Hiki ambae Pia ni Kamishina wa Kamisheni ya Uchunguzi wa kisayansi amesema mafunzo hayo yatalisaidia kuwa jenga askari kiutendaji na kuleta ufanisi ndani ya Jeshi la Polisi hususani kwenye suala zima la kuboresha mawasiliano katika kukabiliana na Majanga na dharura Kulingana na Mabadiliko ya sayansi na Teknolojia,alisema Kamisha Hiki.