Na Joyce Kasiki,TimesMajira online,Dodoma
WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kauli moja bila kujali itikadi za vyama vyao kwa kauli wamebariki jina la Waziri Mkuu mteule Kassim Majaliwa lililoteuliwa na Rais Dkt.John Magufuli, kuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Tano kipindi cha pili.
Majaliwa amepata kura 350 a ndiyo sawa na asilimia 100 huku kukiwa hakuna kura iliyoharibika.
Wakizungumzia Majaliwa kabla ya kulithibitisha jina hilo kwa kulipigia kura,wabunge wamesema Majaliwa anatosha katika nafasi hiyo na kwamba hayo yamejidhihirisha kwa utendaji wake katika awamu iliyopota.
Mbunge wa Mchinga Salma Kikwete (CCM) amesema,kiteulowankwa Majaliwa ni mwendelezo wa kazi zake zilizotukuka katika awamu iliyopita.
Amesema,Majaliwa ni msikivu,mpole wenye ushupavu wa kusimamia mambo.
Mbunge wa Isimani William Lukuvu amesema amempongeza Rais Magufuli kwa kumuona tena Majaliwa kuwa anaweza katika nafasi na hilo limejidhihirisha wazi kutokana na kazi zake.
“Rais Magufuli ni mtu mwenye maono na amechagua mtu wanayeendana naye sana,amem-tune vizuri na anatekeleza kazi zake vizuri kuliko watu walivyodhani,”amesema Lukuvi.
Kwa upande wake Mbunge wa Newala Mjini George Mkuchika amesema Majaliwa ni mstaarabu anaheshimu kila mtu,ni msikivu na kwamba amefanya mambo mengi ya kulisaidia Taifa ikiwa ni pamoja na kurejesha mamlaka ya mkonge serikalini.
Mbunge wa Momba David Silinde amesema Majaliwa ana uwezo wa kusimamia maono ya Rais Magufuli katika kubadilisha nchi.
Vilevile amesema ana uwezo wa kuunganisha nchi nzima kupitia Bunge na hivyo kufanya kazi ya rais kuwa nyepesi.
“Kwa uwezo wa Majaliwa na maono ya Rais wetu naamini tutampitisha kwa 100 ili kuliambia Taifa nini tunakwenda kukifanya katika miaka mitano ijayo.
Naye Mbunge wa Bahi Kenneth Nollo amesema hana mashaka na utendaji wa Majaliwa na kwamba bado anatosha katika nafasi hiyo.
“Mimi binafsi pamoja na watu wengi walitarajia kurudi kwa Majaliwa katika nafasi hiyo kwanza mara nyingine kutokana na kazi kubwa iliyofanyika katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ,ana ‘speed’ ya rais katika utendaji wake wa kazi kwa maslahi mapana ya nchi yet.”amesema Nollo.
Spika Job Ndugai amesema uwingi wa kura za Majaliwa ni upendo na imani kubwa kwa kiongozi huyo.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi