December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Majaliwa mgeni rasmi maadhimisho wiki ya utafiti na ubunifu UDSM

Na Mwandishi wetu Timesmajira online

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajia kuwa mgeni katika ufunguzi wa maadhimisho ya saba ya wiki ya utafiti na ubunifu ya chuo kikuu cha Dar es salaam yatakayofanyika Mei 24 hadi 26 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo Makamu Mkuu wa Chuo , Profesa William Anangisye amesema maadhimisho hayo yamebebwa na kauli mbiu ya utafiti na ubunifu kwa manufaa ya kijamii nchini Tanzania.

Amesema katika maadhimisho hayo chuo kikiuu kitaonesha miradi 103 kati ya miradi ya utafiti iliyofanya vyema zaidi kati ya 300 ya mwaka huu

Akitaja miradi hiyo ni pamoj na miradi wa maabara ya kidijitali, glavu maizi kwa wenye matatizo y kusikia na kuzungumza na mtambo maalumu wa kuyeyusha shaba kwa ajili ya wachimbaji wadogo nchini Tanzania.

“Chuo kikuu cha Dar es salaam kitatumia fursa ya maadhimisho hayo kujipambanua katika utafiti ambao ni mojawapo ya majukumu yake makuu, kwa kuonesha shughuli zake za utafiti ,ubunifu huduma kwa jamii na ubadilishaji maarifa kwa njia ya kutatua chagamoto mbalimbali ” alisema

Aidha amesema katika siku ya kwanza ya ufunguzi kutakuwa na wazunguzaji wakuu wawili ambao mfanyabiahara Seif Ali Seif pamoja na mkurungezi Mkuu wa Superdol limited ambaye atatoa mada kuhusu ushirikiano wa sekta ya uzalishaji n vyuo vya elimu ya juu nchini Tanzania .

Mwingine ni Profesa Evelyn Mbede ambaye ni Profesa katika sayansi ya jiolojia kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam ambaye atazungumzia Gesi ya Helium na maendeleo ya viwanda nchini Tanzania.

Vilevile amesema wiki hiyo itatoa fursa ya kuimarisha ushirikiano baina ya chuo kikuu cha Dar es salaam na wadau mbalimbali kitaifa na kimataifa ambapo kutakuwa na mjadala maalumu wa ushirikiano ya kimkakati utakaowashirikisha wadau kutoka katika sekta binafsi na za umma huku ukijikita katika masuala ya viwanda, biashara, ujasiriamali, ubunifu na utafiti.

Katika hatua nyingine Profesa Anangisye amesema wiki hiyo ya maadhimisho pia itatambua michango iliyotukuka ya wanataaluma na wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam katika utafiti,ubunifu na ubadilishanaji wa maarifa.

Amesema Mei 26 Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia Profesa Adolf Mkenda ambapo atawatunuku tuzo watafiti na wabunifu bora katika makundi ya miradi bora wa utafiti, mtafiti bora, mbunifu bora, miradi bora ya wanafunzi wa uzamili, miradi bora wa wanafunzi wa shahada za awali, miradi bora wa katika kutoa huduma kwa umma, vitengo/idala zilizoingiza kiasi kikubwa cha fedha za utafiti, vitengo/idala zilizoingiza kiasi kikubwa cha fedha za ubunifu pamoja na watafiti waliongiza kiasi kikubwa cha fedha za utafiti.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangiisye (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa kuhusu Wiki ya maadhimisho ya saba ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam yatakayoanza Mei 24 hadi Mei 26,2022 katika eneo la Maktaba mpya katika Chuo hicho