December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Majaliwa atoa siku saba watendaji,TARURA,DAWASA kukamilisha barabara Muhimbili

Na Mwandishi wetu Timesmajiraonline

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa ametoa siku saba Kwa Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Dar es Salaam Godfrey Mkinga na Mkurugenzi wa Usafi wa Usimamizi wa Usafi wa Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingiza (DAWASA) Lydia Ndibalema kukamilisha barabara Muhimbili.

Amesema kuwa siku saba zinatosha na wawe wamekamilisha kipande cha barabara ya Mariki kinachoingia geti kuu la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kiwango cha lami.

Waziri Majaliwa ametoa maagizo hayo leo Julai 24, 2023 alipofanya ziara ya kushitukiza kukagua barabara hiyo ambapo amesema barabara hiyo ambayo ilibomolewa kwa urefu wa mita 60 kupisha matengenezo ya bomba la maji machafu linalotoka hospitali hiyo ilipaswa kuwa imekamilika tangu mwishoni wa mwezi wa sita 2023.

Waziri Majaliwa amewaagiza watendaji hao kufanya kazi usiku na mchana ili kuepusha adha kwa wagonjwa na wanafamilia wanaoitumia barabara hiyo kuelekea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.