Na Mwandishi Wetu.
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameipongeza hatua ya Wizara ya Afya ya kuongeza kasi ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi baada ya kutekelezwa maagizo yake ya kushirikiana na Ofisi ya Mkoa katika kusimamia mradi huo ambayo maagizo hayo aliyatoa mwaka jana 2021 mwezi wa nane .
Katika ziara yake Mkoani Katavi, Waziri Mkuu ametembelea Hospitali hiyo na kukuta ujenzi sasa umefikia asilimia 92 kwa ‘Wing A’ kutoka asilimia 40 mwaka jana.
Akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi amesema kuwa mradi wa Wing A utakamilika 31 Desemba, 2022 na huduma kuanza kutolewa tarehe 01 Januari, 2023 .
Prof. Makubi amesema Ujenzi wa Wing B unategemea kukamilika Oktoba, 2023. Mheshimiwa Waziri Mkuu yupo Mkoani Katavi kwa ziara ya siku mbili.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi