December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

MAIPAC kutoa kompyuta 5 shule ya Arusha Alliance

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Asasi ya MAIPAC inatarajia kutoa kompyuta 5 zenye thamani ya zaidi ya Milioni 7 kwa shule ya awali na msingi ya Arusha Alliance lengo likiwa ni kuwasaidia wanafunzi juu ya teknolojia za kisasa kupitia kompyuta

hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa MAIPAC Musa Juma wakati akiongea na wanafunzi,walezi,na wahitimu wa darasa la saba ambao wameitimu elimu ya darasa la saba wiki iliopita kwenye shule hiyo.

Musa amesema kuwa msaada huo ambao watawasilisha shuleni hapo hivi karibuni utalenga kuwajengea wanafunzi uelewa na teknolojia ambazo wakati mwingine ni muhimu wazijue.

“tutatoa kompyuta hizo ili wanafunzi hata kama wanatoka nje jiji la Arusha nikimaanisha wafugaji waweze kupata uzoefu na kujua matumizi sahihi ya kompyuta hizo”ameongeza Musa

Wakati huo huo ametoa wito kwa walimu hapa nchini kuhakikisha kuwa wanafanyaa kazi zao kwa umakini mkubwa ikiw ni pamoja na kujiwekea utaratibu wa kubuni miradi kama vile ya shule

“leo ni maafali ya 14 ya hii shule lakini historia yake inaonesha kuwa ni umoja wa walimu waliamua kuanzisha mradi wao ambao sasa umezaaa matunda makubwa kwa jamii nawaasa hata walimu wengine nao waweze kujua kuwa kazi yao ni njema sana na kama watakuwa wabunifu basi ni wazi kuwa jamii itasaidika sana”aliongeza

Wakati huo huo mkuu wa shule hiyo, Elimboto Mdiu amewaasa wazazi kuhakikisha kuwa kwa kipindi hiki ambacho wanafunzi wameitimu elimu ya msingi wanapaswa kusimamia maadili kwa kuwa nyakati za sasa mmonyoko wa maadili ni janga kubwa sana

Mdiu amebainisha kuwa mmonyoko wa maadili ni mkubwa lakini kama kila mzazi atasimama na kumpa kazi pamoja na masomo ya kufanya kwa kipindi hiki cha kusubiri matokeo

“wazazi wakisama vema ipasavyo na watoto hawataweza kupotea na badala yake watasimama na kuendeleza kile ambacho sisi tumewafundisha”

Amemalizia kwa kusema kuwa pamoja na kuwa wazazi Wapo kwenye harakati za maisha ya utafutaji wa kila siku ni muhimu kuhakikisha kuwa suala la maadili hasa ya watoto linapewa kipaumbele ipasavyo.