December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mahimbali: Uwekezaji wa madini bado mdogo Afrika

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Madini Nchini, Kheri Mahimbali, amesema Tanzania kwa sasa imeweka mazingira mazuri kwa wawekezaji kuja kuwekeza kwenye sekta ya madini kwa namna itakayofaidisha pande zote.

Mahimbali ameyasema hayo wiki hii wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya madini uliondaliwa na taasisi ya Chatham House na uliofanyika jijini London.

Katika mkutano huo, Katibu Mkuu Mahimbali amezungumzia umuhimu wa kuongezeka kwa uwekezaji kwenye madini ya kimkakati ambayo yako kwa wingi ambao uwekezaji wake umekuwa mdogo ukilinganisha na mahitaji yaliyopo hasa barani Afrika.