January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Magifti dabodabo yaendelea kuwainua wananchi kiuchumi

Novat Freemin Lyaruu Mchoma Nyama Dar Es Salaam, Kumbuka Mbugulu na Jenifer Gunga ni baadhi ya wawakilishi wachache kutoka Dar Es Salaam waliojishindia Milioni Moja Moja na kuingia kwenye Orodha ya zaidi ya Washindi 110 wa kampeni ya MAGIFTI DABO DABO inayoendelea hivi sasa.

Ikumbukwe Kampeni hii inayoendeshwa na Kampuni ya Tigo ilizinduliwa Mwishoni mwa Mwezi Novemba Mwaka jana huku  ikimtambulisha Haji Manara kama SEMAJI la Kampeni hii, ambapo mteja wa Tigo anaweza kushinda Fedha Taslimu hadi Milioni 10, Safari ya Kwenda Dubai au Zanzibar, Set ya Vifaa vya Ndani ambavyo ni Sound bar, Friji, TV na Microwave na Zawadi kubwa ya Magari Mawili ( 0km ) , kingine kinachovutia katika kampeni hii ni kwamba ukishinda kitu kimoja wapo kati ya ivyo unamchagua na yeyote umpendae ili apewe zawadi iyoiyo uliyoshinda hii ndio maana halisi ya MAGIFTI DABO DABO.

Akizungumza baada ya kuwakabidhi washindi mfano wa Hundi Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi. Mary Rutha  amewasisitiza  Watanzania kufanya miamala mbalimbali na Tigo Pesa ili kuibuka washindi wa Pesa Taslimu, Vifaa vya Hisense na Zawadi kubwa ya Magari Mawili katika Droo mbilii zilizobakia.

“Mwezi Disemba Tigo tuliwapeleka washindi 15  DUBAI , na wengine walienda Zanzibar katika kampeni hii hii” wapo pia waliojishindia Pesa Taslimu na wapo pia wamejishindia Vifaa vya Hisense. kwahyo kampeni bado inaendelea fanyeni miamala na TIGO PESA kwa wingi, Lipa kwa Simu, nunua vifurushi ili utengeneze mazingira ya kuibuka Mshindi ” amesema Mary Rutha.

Kwa upande wa washindi Novat Freemin Lyaruu Mchoma Nyama Jijini Dar Es Salaam amesema pesa aliyoipata atanunua mbuzi wa kutosha suala litakalomwezesha kupanua BIASHARA yake, naye Mshindi Jenifer Gunga Mkazi wa Kisarawe amesema alikua ana ndoto ya kufungua saluni kwahiyo MAGIFTI DABO DABO imemtimizia ndoto yake.