January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Maganga aeleza utekelezaji wa Ilani Zingiziwa

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Diwani wa Kata ya Zingiziwa Maige Maganga, ameeleza utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM alivyosimamia miradi ya maendeleo.

Diwani Maige Maganga, alisema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Zingiziwa na Chanika jimbo la Ukonga, mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa mkoa Dar es Salaam Albert Chalamila.

“Katika kata ya Zingiziwa inapata maendeleo makubwa katika usimamizi wangu wa uongozi wa Diwani kulikuwa amna kituo cha afya sasa Zingiziwa Serikali imejenga kituo cha afya cha kisasa kwa shilingi milioni 570,na zahanati ya Zogoali imejengwa na kituo cha afya Chanika kitakuwa Hospitali kamili shule ya Msingi GOGO imekuwa ENGLISH Medium “alisema Maige.

Diwani Maige Maganga alisema pia katika uongozi wake ametekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM kwa kujenga shule mbili mpya za msingi Zogoali na kibadeni kwa milioni 700 ili wanafunzi waweze kusoma karibu na makazi yao kutoka jiographia ya eneo la kata ni kubwa hivyo ameweza kusogeza huduma za jamii karibu na wananchi wake .

Soko la Zingiziwa zilitumika shilingi milioni 107 kwa ajili ya ujenzi wake wa awali soko hilo linaendelea kujengwa.

Mafanikio mengine Barabara kuwango cha lami Homboza kwa makamu wa Rais Chanika anbayo sasa hivi ujenzi wake umekamilika wananchi wanatumia.

Akieleza changamoto za Zingiziwa vivuko vya Lubakaya ,kwa mama Yusuph,changamoto zingine vibari vya ujenzi waandisi wa Halmashauri wanaenda Zingiziwa kuchukua pesa za vibari vya ujenzi na baadhi ya Watendaji wanakamata wananchi wake kwa tojo ya taka.

Aidha pia alisema katika Suala la urasimishaji makazi toka mwaka 2019 Kamati ziliundwa zikachukua pesa na Wakandarasi wa mradi wakachukua pesa hati mpaka leo bado .

Alitumia fursa hiyo kumpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji Jomaary Mrisho Satura, Naibu Meya Ojambi Masaburi na Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jery Silaa amefanikisha mradi wa Umeme wa REA Mtaa wa Somelo wakati wowote wananchi wanawekewa umeme .

Aliwataka wananchi wa Zingiziwa kuunga mkono juhudi za Serikali za kuleta maendeleo ambazo zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Zingiziwa imekuwa ya kisasa huduma zote za kijamii zipo,ikiwemo vituo vya afya,Soko ,Barabara, sekta ya Elimu yote hayo yamefanywa na Serikali.