Na Penina Malundo,Timesmajira
MKUU wa Chuo cha Mafunzo ya Juu ya Kijeshi Kunduchi,Meja Jenerali Suleiman Mzee amefungua Kozi ya siku tano ya Uongozi kwa viongozi waandamizi wa Ulinzi wa Amani kutoka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC),Vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na Taasisi za Serikali za kiraia kutoka Tanzania huku akiwataka kushiriki mafunzo yanayotolewa kikamilifu.
Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam,wakati wa ufunguzi wa Kozi hiyo,alisema kozi hiyo itawasaidia viongozi hao waandamizi wa Ulinzi wa Amani katika utekelezaji wa majukumu yao.
Amesema ni muhimu nchi wanachama wa SADC kujitahidi kushiriki katika mafunzo mbalimbali yanayotolewa kuhusiana na ulinzi wa amani ili kupata uelewa wa pamoja ambao utakuwa nguzo muhimu katika utekelezaji wa majukumu yao.
Meja Jenerali Mzee alisema kuwa viongozi hao wanapopata mafunzo hayo kwa pamoja wanapata uelewa mmoja wa kutekeleza majukumu yao.”Nasisitiza wale wanaoashiriki kwenye jukumu la ulinzi wa amani wakipata mafunzo haya yatawasaidia kufanya majukumu yao kwa weledi na ufanisi mkubwa,”amesema.
Amesema katika nchi zetu na duniani kumekuwa kukijitokeza na changamoto ambazo zinasababisha watu kuuawa na kushambuliana, hivyo chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa (UN) zipo juhudi za kulinda amani ambazo zinmegawanya katika kanda.
Meja Jenerali Mzee amesema kwa Afrika ukanda ni SADC ambapo kupitia mafunzo hayo yamewakusanya wajumbe kutoka nchi hizo wanakutana na kupewa kozi hiyo.
Kwa Upande wake Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani Tanzania, Brigedia Jenerali George Itang’are amesema kozi hiyo ni kubwa kuliko zote zilizoendeshwa kwa walinzi wa amani na kwa mara ya kwanza inatolewa nchini na ni kozi ya pili Kikanda.
“Kozi hii ya leo ni ya kwanza kufanyika hapa nchini Tanzania na lengo kubwa ni kutoa fursa kwa maofisa wakuu ambayo wataenda kwenye ulinzi wa amani katika nchi mbalimbali chini ya UN na SADC kupata uelewa wa pamoja,” Amesema
More Stories
Mo Dewji na Urithi anaoujenga ,unavyoenda mbali zaidi ya mafanikio binafsi
Mulika Community kusaidia Serikali kukomesha vitendo vya ukatili
TMDA yashinda tuzo za PRST ya Umahiri katika kampeni bora ya utoaji elimu jamii