November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mafanikio ziara ya Rais Samia Morocco, Saudi Arabia yaanikwa

Na Mwandishi Wetu,TimesMajiraOnline,Dar

ZIARA za Rais Samia Suluhu Hassan katika nchi mbili za Morocco na Saudi Arabia, zimekuwa na mafanikio makubwa, ambapo pia alitumia mkutano wa Jukwaa la Uwekezaji Afrika, mradi wa ujenzi wa reli kutoka Mtwara hadi Mbamba Bay na matawi ya Liganga na Mchuchuma yenye urefu wa kilomita 1,000,kunadi.

Mafanikio ya ziara hizo mbili yalielezwa na Ikulu jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunusi, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Rais Samia amefanya ziara hizo mbili kuanzia Novemba 8 hadi 11, mwaka huu.

Amesema Mradi huo una lengo la kuufungua ukanda wa Kusini wenye madinimbalimbali ambayo ni Makaa ya Mawe kutoka Mchuchuma, Chuma cha Liganga, Graphite na saruji.

“Mradi huu unaenda sambamba na uimarishaji wa bandari ya Mtwara, Ujenzi wa Kongani za viwanda na Tanuru ya kuchenjua madini
(Smelter).

Mradi huu ni miongoni mwa miradi ya reli ya vipaumbele
inayotekelezwa nchini na ni kati ya miradi ya Ukanda wa Kusini (Mtwara Development Corridor) inayolenga kujenga Miundombinu ya
kuunganisha Nchi za ukanda wa Kusini mwa Afrika yaani Tanzania,
Malawi, Msumbuji na Zambia.

Pili, Zuhura amesema nchi yetu imefanikiwa kuunadi mradi wa Mangapwani Multiporpose Port – Zanzibar.

Amesema huo ni mradi wa Bandari wa Mangapwani unaohusu
ujenzi wa Bandari jumuishi ya kuhudumia meli za mizigo ya makontena na kichele zenye uwezo wa kubeba uzito unaofikia tani 200,000.

Mradi huu kwa awamu ya kwanza umekadiriwa kutumia dola za Kimarekani Milioni 400. na utatekelezwa kwenye eneo
la Mangapwani lililopo kaskazini mwa eneo la bandari ya Malindi
inayotumika hivi sasa.

Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetenga eneo la hekta zaidi ya 900 kutekeleza mradi huu jumuishi wa Bandari. Eneo hilo pia linajumuisha ujenzi wa bandari ya huduma za utengenezaji wa meli, ujenzi wa maeneo huru ya biashara “(free zone) ikiwemo miundombinu ya barabara, maji, umeme na majengo ya viwanda na maghala ya kuhifadhia bidhaa.

Mradi huu ukitekelezwa utasaidia kuwa bandari kuu ya uletaji mizigo ukanda wa eneo la Afrika Mashariki kwa kuwa eneo unapotekelezwa ni lenye kina kirefu cha maji yaani (mita 17 maji madogo na mita 25 maji makubwa) na kuwa bandari inayohudumia kontena katika ukanda huu wa EAC.

Kulingana na utabiri wa kiasi cha mizigo inayotarajiwa
pamoja na hali na mwenendo wa maendeleo ya biashara ya usafirishaji mizigo kwa meli za dunia na Afrika, bandari hii itaweza kuhudumia meli zenye uwezo wa kubeba uzito wa tani 30,000 hadi 100,000.

Zuraha amesema ilihitimishiwa nchini Saudi Arabia, ambako ulifanyika mkutano wa masuala ya uchumi kati ya Saudi Arabia na mataifa ya Afrika mjini Riyadh.

Amesema Taasisi ya Mfuko wa Maendeleo ya Saudia imewekeza kiasi cha dola za kimarekani milioni 533 kwenye mataifa ya Afrika na Tanzania ikiwemo.

Amesema Rais Samia alishiriki katika mkutano huo na viongozi mbalimbali walishiriki katika mkutano na wawekezaji wa Saudi Arabia (Round Table meeting) ambapo pia kampuni mbalimbali zilishiriki.

Amesema miongoni mwao ni Kampuni ya Almarai ambayo ipo tayari kuja nchini na kuanzisha mradi wa uzalishaji majani kwa ajili ya kulisha mifugo.

“Itakumbukwa kwamba kampuni hii ilishaanza mazungumzo na Wizara
ya Mifugo kwa ajili ya kuanzisha mradi huo. Kampuni nyingine zilizoonesha nia ni pamoja na kampuni ya Salic, kampuni ya Crown Agricultural ambayo nayo inalenga kuanzisha mradi wa kilimo cha majani ya kulishia mifugo (Alfa alfa) na mradi wa kunenepesha ng’ombe na kuuzwa katika soko la mashariki ya kati,” alisema.

Aidha, mkutano huu umewezesha nchi yetu kutambua kuwa lipo soko
kubwa la nyama nchini Saudi Arabia ambapo Somalia wamefaidika kwa
kupeleka nyama ya mbuzi Tani laki 5 kwa mwaka.

“Hii ni fursa kwa Tanzania kutumia nafasi hii kuzalisha na kuuza nyama ya mbuzi ambayo ni bora zaidi, nchini Saudi Arabia.
Fursa nyingine zilizowasilishwa na ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Rais Samia ni Uwekezaji katika biashara ya maziwa,” amesema.

Amesema uwekezaji katika biashara ya ufugaji samaki, uwekezaji katika sekta ya Madini, Kilimo, mahoteli, viwanda na Tehama.
Na pia Tanzania imefanikiwa kupata Soko la Ajira za Wafanyakazi na
Wafanyakazi wa Ndani- na MoU yaani hati za makubaliano tayari
zimesainiwa.

Kwenye Nishati Tanzania imefanikiwa kupata Mkopo wa Bilioni 33 kwa
ajili ya Umeme – Benako Kyaka na ahadi ya kushiriki kuwekeza