Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Hassan Suluhu amemaliza ziara katika Mkoa wa Songwe akiwa njiani kuelekea Dodoma kwa Kurejesha Tabasamu kwa wakazi wa Jimbo la Tunduma na Mbozi waliofika barabarani Kumlaki akiwa njiani kuelekea mkoani Dodoma.
Shamrashamra za Wananchi wa Tunduma na Mbozi katika mapokezi ya Rais Samia zilitoa nafasi ya kusikiliza kero, kupongezana kwa miradi iliyotekelezwa pamoja na maelekezo mahususi kwa watendaji wa serikali na chama ndani ya Mkoa wa Songwe.
Aidha Rais Samia amewezesha tabasamu kwa kugharamia matibabu ya mtoto anayesumbuliwa na ugonjwa wa moyo, ununuzi wa mguu wa bandia kwa mwanafunzi wa shule ya msingi pamoja kijana aliyepata ajali na kukatika mkono na mguu yeye atapata mkono na mguu wa bandia kunuwezesha kufanya kazi zake.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewashukuru wakazi wa Mbozi na Tunduma na Mkoa wa Songwe kwa ujumla kuwakumbusha kulinda Amani, ulipaji wa kodi kwa wakati pamoja na kuwarejesha kuwa awamu ya Sita inakwenda na falsafa za 4R hivyo ataendelea kuzisimamia.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato