Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Rungwe
MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya wameridhishwa na utendaji kazi wa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo,Renatus Mchau na kukubaliana shule mpya ya Ufundi inayotarajiwa kujengwa kuitwa jina la mkurugenzi huyo kama sehemu ya kuenzi utendaji wake ulioleta matokeo yenye tija kwa wilaya hiyo.
Madiwani hao wamefikia makubaliano hayo baada ya kujiridhisha mabadiliko yaliyoletwa na Mkurugenzi huyo ikiwemo kuongezeka ufaulu wa shule za Sekondari na kumaliza tatizo la vifo vya mama na mtoto katika Halmashauri hiyo kwa muda wa miezi Saba.
“Haijawahi kutokea halmashauri hii kutokuwepo watoto wenye zero,lakini Sasa hivi wanafunzi wamefaulu daraja la kwanza na la pili shule zote za Sekondari,huyu Mkurugenzi ameleta Mabadiliko makubwa sana lazima aache alama kwenye wilaya yetu kila eneo amegusa maeneo yote”amesema Elizabeth Ngaga Diwani kata ya Ndanto .
Azimio hilo limefikiwa baada ya Kamati ya Huduma za Jamii chini ya Mwenyekiti wake Emmy Maseta kuliomba Baraza hili kupokea pendekezo na kuidhinisha jina la shule hiyo tarajiwa kusajiliwa kwa jina la Renatus Mchau.
Hata hivyo inaelezwa kwamba serikali chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi Mil.500 kwa ajili ya Ujenzi wa shule hiyo ya Ufundi ambayo inatarajiwa kujengwa katika kata ya Kisondela.
Hata hivyo Diwani Maseta amelieleza Baraza hilo la Madiwani kuwa tangu Mkurugenzi huyo aanze kazi katika wilaya ya Rungwe imeshuhudiwa miradi mingi ya Elimu na Afya ikikamilika kwa wakati hatua iliyoongeza upatikanaji wa huduma karibu kwa wananchi.
Aidha kutokana na Ubora ya miundombinu ya elimu kwa sasa ufaulu umepanda kwa mitihani ya taifa ambapo kwa elimu ya Msingi na Sekondari ufaulu umefikia asilimia 94 -100%
Pamoja na hayo Matokeo ya kidato cha sita 2024 imeshuhudiwa daraja la nne na sifuri likitupiliwa mbali hatua iliyotokana na Mchau kusimamia upatikanaji wa vifaa vya kufundishia, motisha kwa walimu,udhibiti wa nidhamu na uboreshaji wa mazingira ya kusomea na kujifunzia.
Mkurugenzi huyo alianza kuwatumikia wakazi wa wilaya ya Rungwe mwaka 2021 akitokea katika Halmashauri ya Kilwa ambako pia alihudumu katika nafasi hiyo aliyonayo sasa.
Jumla ya shule Mpya saba za sekondari zimejengwa katika kipindi chake ambazo ni (Kyobo, Isaka, Msasani, Kikota, Lupepo, Isaka na Lukata) na Shule za Msingi 4 ambazo ni Chifu Mwanjali, Kibumbe, Ushirika na Umoja. Vituo vya afya (8) ni pamoja na Ndanto, Iponjola, Kyimo, Masebe, Malindo, Kinyala, Masoko, Kiwira
Zaidi ya hayo Mchau amefanikisha ujenzi wa Stendi mpya ya Mabasi katika Mji wa Tukuyu kwa kiwango cha Paving Blocks na Zege, Ununuzi wa Gari jipya la Taka na na dogo kwa ajili ya shughuli za Utawala pamoja uanzishwaji wa Kituo (Packhouse) jumuishi cha Mazao ya Matunda (Parachichi) katika kata ya Nkunga ambapo ujenzi wake unatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Ujenzi wa soko la Kisasa la ndizi katika kata ya Kiwira (Karasha) nao unatarajiwa kuanza hivi karibuni mara taratibu zitakapokamilika.
Katika hatua nyingine katika kipindi chake Mchau amefanikisha ukusanyaji wa mapato ya ndani kutoka Billion 5.3 Mwaka 2021 Mpaka kufikia Bilioni 7.4 Mwaka huu 2024 hatua iliyosaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya afya,elimu, Usafirishaji, Motisha kwa watumishi pamoja na ununuzi wa vitendea kazi mbalimbali vya serikali.
Baadhi ya miradi iliyotekelezwa kwa mapato ya ndani ni pamoja na ujenzi wa shule mpya ya Umoja na Ushirika, Zahanati ya Lufumbi pamoja na kituo cha afya Kinyala, Malindo , Masebe pamoja na ujenzi wa stendi ya mji wa Tukuyu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Renetus Mchau amewataka watumishi kuwa waadilifu ili waweze kutoa huduma kwa weredi na kuzingatia Kanuni za utumishi Hali itakayochochea matokeo chanya.
Mchau amesema wilaya hiyo itazidi kusonga mbele iwapo kila mmoja ataweza kufanya kazi zake kwa weredi.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best