Na Esther Macha, Timesmajira, online, Mbarali
UONGOZI wa halmashauri ya wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya umesema kuwa serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kwa ajili ya utengenezaji wa barabara lakini bado kuna wananchi ambao wamekuwa wakibomoa barabara na kupitisha mifereji ya maji mashambani na ifike wakati madiwani kukemia na kuwa wakali dhidi ya vitendo hivyo na si kuwaacha kwa kigezo cha kulinda kura .
Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbarali , Twalibu Lubandamo wakati wa kujadili bajeti kwa miaka mitatu 2023/2024-2025/2026 na makisio ya mapato na matumizi kwa mwaka
2023/2024.
Lubandamo amesema kuwa kwa wananchi ambao wanabomoa miundombinu iliyotengenezwa na serikali ni maadui wa serikali na hata kama mwananchi anafanya uharibu wa barabara kwa kigezo cha kuwa alikupigia kura sio sawa.
“Ninaomba twende tukawajibike kwa sehemu yetu tuwe wakali kwa wananchi serikali inatengeneza barabara wao wanaennda kubomoa ninawaomba madiwani hata kama hawa watu wapiga kura nenndeni mkawe wakali hawa ni maadui zetu kwenye utawala wetu , hii Mbarali karibu sehemu kubwa miundo mbinu iliyotenezwa mwaka jana tu mwaka huu tu imechimbwa haifai kabisa “amesema.
Akizungumzia kuhusu mifugo Lubandamo amesema mifugo imekuwa ikipitishwa barabarani ng,ombe karibu 500 inapitishwa barabarani hivyo ni vema madiwani wakatoe elimu kwa wananchi wao na kusema
sheria za mifugo zipo wazi kwani mifugo inapokwenda umbali fulani inatakiwa kupakiwa kwenye magari ili iweze kupita .
“Sisi madiwani tuwe sehemu kubhwa ya kutoa elimu kwa wananchi kwani sisi sote hapa tunafahamu sheria za mifugo hivyo nawaomba tuwe mabarozi wazuri kwa wananchi wetu kama mlivyosikia hapa kwenye taarifa ya Mhandisi wa Tarura kuwa mifugo inasambaa sana barabarani “amesema Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Itamboleo.
Mhandisi Anyitike Kasongo ni Meneja wakala wa barabara wa barabara vijijini wilaya ya Mbarali (TARURA)amesema kuwa kumekuwa na changamoto nyingi wakati wa utekelezanji wa agizo la serikali ambapo walikata baadhi ya barabara wakati wa kuongeza maji mto Ruaha ambapo kuna barabara mbili ambazo zimeathiriwa sana ambayo inahitaji mil.250 kwa ajili ya Daraja .
Aidha amesema changamoto nyingine ni upitishaji wa mifugo kwenye barabara hivyo kuharibu barabara kutokana na kupitisha makundi makubwa ya ng,ombe 200 mpaka 1000 .
Pia amesema wakulima wakati wakiendelea na shughuli za kilimo wamekuwa wakielekeza maji kwenye barabara hivyo kuathiri miundo mbinu .
wakulima wanalima mashamba mpaka kwenye kingo za barabara hali inayofanya miundo mbinu kutodumu kutokana na maji kuwa mengi .
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbarali , Missana Kwangura amesema kuwa katika kuhakikisha miundo mbinu ya wilaya hiyo inaendelea kuwa vizuri atashirikiana na madiwani katika kutoa elimu kwa wananchi ili uharibu huo usiendelee kuwepo.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini