December 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Madiwani Ilala watoa tamko 2025 Sultan Obama aendelee Udiwani

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Madiwani wa Jimbo la Ilala wametoa tamko lao mwaka 2025 DIWANI anayetosha Upanga Mashariki Sultan Salim (OBAMA wa UPANGA ) aendelee nafasi ya Udiwani wa kata ya Upanga Mashariki .

Madiwani hao wa Jimbo la Ilala walisema Sultan Salim (OBAMA )ni Mwalimu wao ndio amewafundisha siasa zote mpaka wamefanikiwa kupata Udiwani katika kata zao .

Akizungumza wakati Diwani Sultan Salim Obama wa UPANGA akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi ya Upanga Mashariki ya January 2022 mpaka January 2023 Diwani FATUMA ABUBAKARI alisema sultani ni mchapa kazi ana Mahusiano mazuri na chama na Serikali pamoja na wananchi wake .

Diwani Fatuma alisema toka 2015 Sultani Diwani wa Upanga Mashariki mpaka Sasa wanamuombea Dua aendelee mpaka 2025 .

Diwani wa Kata ya Upanga Magharibi Adinan Kondo alisema Diwani Sultan Salim Obama wa UPANGA ni Mwalimu wake wa Siasa amempa Elimu na mbinu mbalimbali za Siasa katika Kampeni za Uchaguzi kamsaidia mpaka amepata udiwani Upanga Magharibi .

Diwani Adinan alisema Sultan anafanya kazi kwa weledi amekuwa Mshauri wao katika vikao mbalimbali vya Serikali na chama.

Diwani wa Kata ya Kivukoni Sharick Choughule amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Mbunge wa Jimbo la Ilala Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu na Diwani Sultan Salim kwa Utekelezaji Ilani kwa vitendo .

Diwani Viti Maalum Wanawake Ilala Batuly Mziya alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuelekeza pesa za Maendeleo Jimbo la Ilala Sekta Elimu ,Afya na Miundombinu ya Barabara na kuwataka Wana CCM kuunga mkono Juhudi za Mwenyekiti wa CCM TAIFA Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Aidha pia amempongeza Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu kwa kusimamia miradi ya Maendeleo pamoja na Diwani Sultan Salim kwa kuwashirisha Ilani ya chaama katika Halmashauri kuu ya Kata.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Upanga Mashariki Josephine Burengelo.

Alisema Diwani Sultan ni sawa Daimond anatosha atakuwa Diwani wao miaka yote awaongoze Upanga Mashariki .

Mwenyekiti Josephine alisema baada kuona Sultan miaka yote anaongoza Udiwani vizuri mahusiana chama ,Serikali pamoja na Wananchi mazuri ndio akalazimika kuchukua fomu ya kugombea Nafasi ya Mwenyekiti wa CCM kata ambapo amefanikiwa kushika kiti hicho katika Uchaguzi wa chama .

Kaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala Jesca Msengi aliwataka Wana CCM na Makada wa chama hicho kuwapa Ushirikiano madiwani na Wabunge katika kufanya kazi za maendeleo na Utekelezaji wa Ilani muda wa muda wa kampeni kugombea ujafika .

Kaimu Katibu wa Wilaya Jesca aliwataka Wana CCM wafanye mahusiano ya chama na Serikali vizuri washikamane.

DIWANI wa Upanga Mashariki Sultan Salim (katikati)akikabidhi Ilani ya Chama kwa Kaimu Katibu wa Wilaya ya Ilala (Kulia )Jesca Msengi na Mwenyekiti wa CCM Upanga Mashariki Josephine Burengelo (Picha na Heri Shaaban )
Diwani wa Viti Maalum Wanawake WIlaya ya ILALA Batuly Mziya Akizungumza katika kikao UPANGA Mashariki wakati Diwani Sultan akiwasilisha Taarifa ya Ilani ya Utekelezaji ya chama (Picha na Heri Shaaban )
DIWANI wa Viti maalum Wanawake Wilaya ya Ilala Moza Mwano akizungumza Katika Kikao Wakati Diwani wa UPANGA wa mashariki Sultan Salim alipokuwa akiwasilisha Ilani ya Chama
Diwani wa Kata ya Kivukoni Sharick Choughule Akizungumza katika kikao Cha Uwasilishaji wa Ilani Kata ya UPANGA Mashariki (Picha na Heri Shaaban )
Diwani wa UPANGA Mashariki Sultan Salim Akizungumza wakati wa kuwasilisha Ilani ya Chama ya mwaka 2022 mpaka January 2023 (Picha na Heri Shaaban).