December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Madereva wanaoendesha magari ya serikali wapewa utaratibu

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Hayo yametolewa Leo Januari 29. 2022 katika chuo cha ufundi Arusha na Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi SP-SOLOMON MWANGAMILO wakati akitoa elimu kwa madereva hao.

Aidha SP Solomon Mwangamilo amewataka madereva wa serikali kuwa wazalendo namba moja nakuvichukulia vyombo hivyo kama vyao na kufuata sheria za sheria za usalama ili kupunguza ajali na kuwa mfano bora kwa madereva wengine

Nae mwenyekiti Bw.Charles Peter ameiomba serikali kuangali kwa mapana masilahi ya madereva wa serikali ambayo amesema kwa namna moja ama nyingne yataongeza chachu ya utendaji wa kazi zao za kila siku.Amewataka wakuu wa idara kuwaruhusu madereva kuhudhuria mafunzo haya pindi nafasi inapotokea ilikuboresha utendaji wa kazi

Pia amesema kuwa madereva hao wamepewa dhamana kubwa na serikali ya kuendesha magari hayo yenye dhamani kubwa sambamba na hilo amesema kuwa kumekuwa na lawama nyingi kutoka kwa watu kuhusu madereva wa serikali kuvunja sheria za usalama Barabarani na kusababisha ajali

Nao baadhi ya madereva walio shiriki mafunzo hayo wameshuru kupata mafunzo hayo kutoka kwa Jeshi la Polisi ambayo wamesema yamewajengea uwezo mkubwa.