October 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Madereva bajaj, bodaboda: Hatutaandamana

Na Nathaniel Limu,TimesMajira Online. Singida

MADEREVA bajaj na boda boda mkoani hapa, wamesema hawatashiriki maandamano wala funjo za aina yoyote kwa kile walichodai Uchaguzi Mkuu kwa ujumla umafanyika kwa haki na uhuru mpana.

Wamesema matokeo ya kujivunia kwa upande wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), hayana ubabaishaji wa aina yo yote, bali yamechangiwa kwa asilimia mia moja na utendaji uliotukuka wa Rais Dkt. John Magufuli.

Hayo yamesemwa juzi kwa nyakati tofauti na Mwenyekiti wa bodaboda, Abudul Mtingo na Mwenyekiti wa bajaj Ahmed Juma, wakati wakitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari.

Mtingo amesema wamekutana pamoja na madereva wa bodaboda na kutoa tamko kwamba wao, hawatathubutu kuingia barabarani kufanya maandamano yasiyo na uhalali wowote.

“Madereva wa bodaboda na Watanzania bila kujali itikadi zao za kisiasa ni mashuhuda wazuri kwamba Uchaguzi Mkuu mwaka huu, uliboreshwa na umefanyika kwa amani na utulivu mkubwa,” amsema Mtingo na kuongeza;

“CCM imebebwa na utendaji na uzalendo wa Rais Magufuli na si vinginevyo, hivyo niwaombe Watanzania wote wenye nia njema na nchi yao, wasikubali kurubuniwa na watu wenye nia ovyo”.