Na Heri Shaaban , TimesMajira Online
UONGOZI wa Machinga Complex, kwa kushirikiana na Wafanyabishara wa Machinga Complex, na Wakandarasi wa Kampuni za Taka SATEK na KAJENJERE wamefanya usafi kata ya Ilala kwa ajili ya kuipendezesha Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam.
Usafi huo wa mwisho wa mwezi Kata ya Ilala Kanda namba mbili uliongozwa na Meneja wa Soko la Machinga Complex Stella Mgumia na Afisa Mtendaji wa kata ya Ilala Vumilia na maafisa afya wa Ilala kwa kushirikiana na Wenyeviti wa Serikali za mitaa Hajj Bechina.
Akizungumza katika kampeni hiyo ya usafi Meneja wa soko la Machinga Complex Stella Mgumia, amesema usafi wa leo ulianzia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Barabara ya Kawawa na Masoko ya Machinga Complex na Kalume sasa hivi maeneo hayo yote yanavutia kwa usafi kwani wamepata ushirikiano mkubwa kwa wakandarasi wa kampuni hizo na wafanyabishara.
“Machinga Complex ni utaratibu wetu kila mwisho wa mwezi tunajumuika na Wafanyabishara na Wakandarasi wa kampuni za taka katika kuipendezesha Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam ususani wilaya yetu ya Ilala “amesema Stella.
Stella amewataka wafanyabishara kujenga tabia ya usafi na kuzibua mitalo katika maeneo yao ya biashara kwa ajili ya kuweka masoko ya machinga komplex katika hali ya usafi “alisema Stella.
Stella amezipongeza kampuni za usafi SATEK na KAJENJERE wanashirikiana vizuri katika masuala ya usafi ambapo alisema kutokana na ukubwa wa Ilala sasa hivi wanafanya usafi kila kanda wamegawana na viongozi wa kanda hizo .
Kampeni ya Pendezesha Dar es Salaam imeifanya Halmashauri hiyo ya jiji la la Dar es Salaam kuibuka kidedea na kushika nafasi ya sita kwa majiji katika usafi
More Stories
Kamati ya Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini yagawa vifaa vya ujenzi
Hatma mrithi wa Kinana kupatikana
Mrithi wa Kinana CCM kujulikana katika Mkutano Mkuu wa Jan 18/19