Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Innocent Bashungwa amekagua maandalizi ya Ufunguzi wa Maonesho ya Bidhaa na Huduma zinazotolewa na kuzalishwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kupitia Vikosi, Makambi, Shule na Vyuo Stadi Pamoja na Shirika lake la Uzalishaji Mali (SUMAJKT) katika eneo la SUMAJKT House Medeli East Dodoma.
Akizungumza jijini Dodoma,Waziri Bashungwa ameonyesha kuridhishwa na maandalizi hayo huku akisema mgeni rasmi katika maonyesho hayo yanayoanza Julai Mosi mwaka huu anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango huku katika kilele cha maadhimisho hayo Julai 10 mwaka huu Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kuwa mgeni rasmi .
“Tunaenda kwenye kilele cha kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JKTB ambalo lilianzishwa Julai 10,1963 na Julai 10,mwaka huu tutakuwa tuna adhimisha miaka 60 ya kuanzishwa kwake,tunamshukuru Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwezesha majsegi yetu kutimiza wajibu wao wa kuhakikisha ulizni wa mipaka yetu unakuwa salama na watanzania tunaendelea kufanya shughuli zetu za uzalishaji mali pamoja na mambo yote ndani ya nchi yetu tukiwa salama,”amesema Waziri Bashungwa
Waziri Bashungwa ametoa wito kwa wanancji wa jiji la Dodoma kujitokeza kwa wingi katika maonyesho hayo na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na JKT.
Kwa upande wake Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema katika wiki hiyo kutakuwa na maonyesho mbalimbali ya bidhaa zinazozalishwa na vikosi vya JKT pamoja na shughuli zinazofanywa na kampuni za Jeshi hilo huku akisema pia kutakuwa na bidhaa zitakazouzwa katika maonyesho hayo.
“Katika maonyesho hayo kutakuwepo wanyama wa porini, vikundi na burudani ,pia wananchi wataelimishwa kuhusu shughuli zinazofanywa na JKT ambazo ni pamoja na kilimo Uvuvi na ufugaji ,lakini pia tumeweka eneo la kuonyesha jinsi JKT linavyowasaidia vijana na nini wanapata .”amesema Meja Jenerali Mabele
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato