January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Maafisa Afya Mkoa wa Dodoma wasisitizwa kusimamia suala la usafi kuweka Jiji katika hali ya nzuri

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

KAIMU Mkurugenzi idara ya kinga Wizara ya  Afya,Dkt.Beatrice Mtayoba amewataka Maafisa afya wote jijini Dodoma kusimamia suala la usafi wa mazingira ili kupunguza maambukizi ya magonjwa ya mlipuko kwa asilimia 70.

Dkt.Mtayoba amesema hayo jijini hapa leo,Novemba 16,2022 alipotembelea katika Soko la Bonanza,lilipo kata ya Chamwino akiongozana na Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma,Prof.Davis Mwamfupe,Diwani wa Kata ya Chamwino,Jumanne Ngede,maafisa afya na kufanya usafi katika eneo hilo la Soko pamoja na wafanyabiashara na wananchi wa maeneo hayo ikiwa ni kuazimisha wiki ya usafi wa mazingira kitaifa ambayo imeanza jana tarehe 15 na na kilele chake Novemba 19, mwaka huu.

Amewataka maafisa hao kusimamia suala la usafi kwa kuhakikisha kuna miundombinu ya usafi kwenye maeneo yote ya masoko kwenye taasisi,kwenye kaya na miundombinu ya vyoo bora na watu wavitumie pamoja na kuweka miundombinu ya kunawia mikono kwa maji tiririka na sabuni.

Aidha amesisitiza maafisa hao kusimamia usafi pembeni ya Kaya mita tano,kwenye mitaro,taasisi,kwenye shule na kuhakikisha kila mtu angalau mita tano inayozunguka eneo lake linakua safi pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kutumia vyombo vya habari.

“Lakini kuna kuna siku zetu tulizotenga siku za jumamosi kufanya usafi,tunamabwana afya,tunawatendaji wa kata lakini kila eneo la Jiji linamwenyewe kwamfano hapa kila eneo tulikokua tunapita hapa mbele ya duka kuna mtaro lakini mbele kuna mwenyewe sasa ile tukiisimamia vizuri tutajikuta kwamba hata kazi zile za jumamosi ya kila mwisho wa mwezi inakua sio nzito,”amesema.

Amesisitiza kuwa usafi wa mazingira ndiyo kila kitu kwani magonjwa yote tunayoyasikia ya Kipindupindu,magonjwa ya Uviko,magonjwa ya ebola yanasababishwa na kutokuwa na mazingira safi.

“Hapa tupo katika msimu wamvua,tunashukuru Mungu mvua bado hazijaanza kwasababu mvua zingeanza kwajinsi ambavyo tumeona mitaro ilivyokuwa imeziba hapa kunachakula tunaenda kwenye msimu wa maembe,kunamatunda,kunandizi,mananasi,kwahiyo kwenye maeneo kama haya ambayo ni maeneo ambayo yanamikusanyiko tuweke msisitizo wa usimamizi,”amesema.

Kwaupande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma,Prof.Davis Mwamfupe amewataka wafanyabiashara wote wa Soko hilo ambao maduka yao mbele kunamtaro na wameweka makalavati kuyatoa na badala yake waweke madaraja ya chuma kwani makalavati yanafanya taka kujificha chini na kushindwa kufanya usafi.

“Watu wote walioweka makalavati humo kwenye mitaro wayavunje na viongozi mlioko hapa mhakikishe kufikia jumamosi tutakapopita tena hapa yawe yamevunjwa badala yake muweke vile vidaraja vya chuma ilituweze kupitisha takataka chini,”amesema.

Pamoja na hayo Prof.Mwamfupe amesema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma limeingia makataba na Kampuni moja kutoka nchini Zimbabwe ambayo lengo lake litakua ni kuchakata taka na kupata gesi na mbolea.

“Badala ya kuziita takataka  zinaenda kuwa mshiko kuna wakati si ajabu tukaona ni lazima tutafute takataka zingine tuziuze kwa namna hiyo,”amesema.

Naye Diwani wa Kata hiyo,Jumanne Ngede amesema kuwa usafi ni jukumu la kila mwananchi nakuhaidi kuendelea kufanya usafi kama ambavyo wamefanya leo.

“Leo tumethibitisha kabisa tumetoka,tunania nzuri yakufanya nchi yet u iwe katika hali salama kwa kata yetu siku ya leo katika maadhimisho ya usafi sisi wanakata ya Chamwino tunahidi kuendelea na usafi,”amesema.