December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Lubandamo: Madiwani endeeleni kuwa pamoja ili kazi za Halmashauri ziweze kusonga mbele

Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbarali

HALMASHAURI ya wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya imesema kuwa Halmashauri nyingi ambazo madiwani wake hawajakaa vizuri kazi zinashindwa kusonga mbele kutokana na Madiwani kutokuwa pamoja.

Imeelezwa kuwa sehemu nyingi ambazo madiwani Wana migogoro Halmashauri zao hazijakaa vizuri kwenye shughuli za kiutendaji sababu wakuu wa idara,watalaam wanashindwa kufanya kazi muda mwingi madiwani wanafika kwa wakuu wa idara na kugombana lakini Mbarali hilo halipo.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbarali na Diwani wa Kata ya Itamboleo ,Twalibu Lubandamo wakati wa mkutano wa baraza la madiwani wa mwaka uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa mkuu wa wilaya.

Aidha Lubandamo amemshukuru Mkuu wa wilaya hiyo,Kanali Dennis Mwila kwa kuwa kiongozi mzuri kwa kutatua migogoro bila kuangalia mgogoro huo unamhusu nani.

“Tunashukuru sana mkuu wilaya wetu tumepata dc aliyenyooka yaani huyu dc ni kama katapila linalokata miti ,nikushuru Sana kuwepo kwako nimejifunza vitu vingi lazima tuongee ukweli dc huyu anatatua migogoro na haangalii huyu ni nani na migogoro inatatulika,ndo maana mtu mkweli sehemu zingine unaweza ukaona wanamchukia wanasema huyu dc aliyekuja Sasa sijui yupoje Mimi nasema kama Mwenyekiti wa halmashauri nasema endelea na utaratibu wako kama kawaida “amesema Mwenyekiti huyo.

Hata hivyo Lubandamo amesema kwamba mkuu wa wilaya Kama wangekuea wanafungua makanisa wangempa uchungaji wa wachungaji ama mchungaji maana yeye ameridhika na kazi aliyopewa na Rais na anafanya kazi kwa ufasaha na simu anapokea kwa mtu yeyote ,na kusema kuwa unapokuwa Mwenyekiti wa halmashauri kuwa na mkuu wa wilaya wa namna hiyo kuna vitu vya kujifunza pia hata Madiwani wanapotatua changamoto kwenye kata zao wajifunze kutoka kwa mkuu wa wilaya.

Akielezea zaidi Mwenyekiti huyo amesema wao kama madiwani wataendelea kushirikiana na wataalamu wetu kwa maana halisi wataalamu ndo wanalinda halmashauri na wataendelea kuwaheshimu na ikitokea kama kuna mtaalamu anataka kuwagawa ataitwa na kusamehewa.

Kanali Dennis Mwila ni mkuu wa wilaya ya Mbarali amewataka Madiwani kuendelea kushirikiana katika kusimamia shughuli za Maendeleo.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Jeremiah Kisangai ambaye pia ni Diwani kata yar Miyomboni amesema inapooneka kuna jambo la kushauri madiwani washauri na kusema kuwa ataendelea kuwa mshauri mzuri wa Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbarali katika kuhakikisha halmashauri inasonga mbele