Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online, Dar
SHIRIKA lisilo la kiserikali la Legal Services Facility (LSF) leo limezindua mpango mkakati wa miaka 5 kufatia kukamilika kwa mradi wa ungwe ya pili 2016 -2020 ulioisha mwaka jana Desemba na kuendelea kwa mwaka mmoja hadi Desemba mwaka huu
Mpanga mkakati huu utatoa dira na mwelekeo wa taasisi hiyo na kuainisha vipaombele vyake zitakavyoweza kusaidia upatikanaji wa haki nchini na kuweka mazingira bora kwa wanawake kupata haki zao na kuchangia katika shughuli za uchumi na kuboresha maisha yao na familia zao kwa ujumla
Aidha mkakati huu umelenga kufanya kazi karibu na serikali na taasisi mbalimbali katika kuboresha sera, sheria na kuweka mazingira bora na wezeshe kwa jamii hususani wanawake
Akiongea wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati , Afisa Mtendaji Mkuu wa LSF, BiLulu Ng’wanakila amesema. “ leo tunayofuraha kuzindua mpango mkakati wa miaka mitano ambao umelenga kutoa mwelekeo endelevu wa shughuli zetu nchini za kuwawezesha wananchi kupata haki zao.
Mpango huu umejikita katika kuchangia mpango wa maendeleo endelevu ya dunia(SDG) SDG 16 uliolenga kuleta haki kwa wote na SDG 5 inayolenga kuboresha usawa wa kijinsia na kuwainua wanawake na wasichana.
Sambamba na malengo endelevu ya dunia pia unachangia katika mpango wa miaka 5 ya maendeleo ya taifa 2016/17-2020/2021.
Mpango wa maendeleo ya taifa 2025 utawala bora, Mpango wa Kitaifa wa Kupambana na Ukatili dhidi wanawake na watoto (NAP-VAWC) huku lengo kubwa likiwa ni kuondoa umaskini na kuchangia katika kuwezesha nchi kufikia katika uchumi wa Kati.
Aidha Ng’wanakilala aliainisha maeneo makuu manne ya kipaumbele na kusema “ “Tunayo maeneo yetu makuu manne katika mpango mkakati ambayo ni (i) kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za msaada wa kisheria,hususani kwa wanawake (ii)Kujenga uelewa kwa jamii juu ya Sheria na haki zao, hususani wanawake (iii)Kuboresha mazingira ya endelevu ya upatikanaji wa haki (iv)kuimarisha taasisi na sekta ya msaada wa kisheria kuwa kuendelevu
.
Tutaendelea kuendesha program hii nchi nzima Tanzania bara na visiwani huku tukiendelea kuyafikia makundi yaliyopembezoni mwa nchi na kutatua changamoto za upatikanaji wa haki maeneo ya mjini na kuendelea kuleta ushawishi na kusaidia mabadiliko na kuundwa kwa sera na sheria bora zitakazoendelea usawa na ushirikishwaji bila kumwacha mtu nyuma katika shughuli za kijamii na kiuchumi
Akiongea wakati wa uzinduzi huo Msajili wa NGO nchini Bi Vickness Mayao amesema amefurahishwa kuona kuwa LSF imekuja na mpango mkakati mpya wa kwa muda wa miaka mitano na kusema kuwa hii inaonyesha wazi kuwa program ya upatikanaji wa haki itaendelea kutekelezwa swala ambalo serikali chini ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto inanufaika kwa kiasi kikubwa na matokeo yake
‘LSF ni mdau wetu mkubwa na moja kati ya NGO zinazofanya kazi kwa karibu sana kwa kushirikiana na wananchi katika kutatua changamoto zinazopelekea wananchi hususani wanawake kupoteza haki zao na wamekuwa wakitoa ruzuku kwa mashirika ambayo mengi tumeshayasaliji sasa kwa mujibu wa sheria . hivyo niwapongeze sana kwa hatua hii Nyingi tunaoyoipiga leo. Tunaamini mpango mkakati huu utaenda kupanua wigo na kuendelea kunufaisha watanzania wengi
Aidha Mayao aliongeza kwa kusema “Wizara ya afya inatekeleza mipango mingi ikiwemo mpango kazi wa taifa wa kudhibiti ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto (NPA-VAWC. LSF kupitia wadau wake na mashirika yanayotoa huduma za msaada wa kisheria yaliyopo kila wilaya yamechangia kwa kiasi kikubwa utekelezaji huu, lakini pia LSF imesaidia kutengeneza nyenzo(tool) ya kufatilia na kureport utekelezaji wake Lakini pia tunashirikiana nao karibu katika kufanya marekebisho ya sera ya wanawake 2000 ambayo pindi itakapokamilika itasadia kulinda maslahi ya wanawake.
Tunaona bado iko haja ya kuendelea kukaa pamoja na kubaini maeneo nyeti ambayo kwa pamoja tukiyafanyia kazi wakati wa utekelezaji wa mpango mkakati huu yataleta tija zaidi”
Nitoe rai kwa wadau mbalimbali ikiwemo serikali kupitia wizara mbalimbali, wadau wa maendeleo, sekta binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali kuunga mkono jitihada hizi na kuwezesha utekelezaji wa mpango mkakati huu kwa kutoa ruzuku au ushirikiano wa kiufundi pale utakapo hitajika. Mwisho niwapongeze wadau wote zaidi ya 200 waliowezesha utekeleza wa mradi huu unaoisha kwa mchango wao mkubwa katika chochea maendeleo endelevu. Aliongeza Mayao
Mpango Mkakati wa LSF 2016-2020 umekuwa ukifadhiliwa na wadau wa maendeleo ikiwemo DANIDA, DFID and EU. Mpango ni kuongeza wadau wengi zaidi ili kuweza kufikia maeneo katika ngazi ya kata na vijiji ambavyo kwa namna moja au nyingine hazikuweza kufikiwa na huduma za msaada wa kisheria bure bila gharama yoyote.
More Stories
Walimu elimu ya lazima watatakiwa kuwa wabobezi kwenye masomo wanayofundisha
Wahakikishiwa usalama siku ya kupiga kura
CCM inabebwa na kazi nzuri za Rais Dkt. Samia-Makalla