January 14, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Lissu na Lema kurudi nchini Tanzania

Na Hadija Bagasha, TimesMajira Online, Tanga

MAKADA Wawili wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Tundu Lissu na Godbless Lema Wamesema wanarudi Nchini Tanzania muda wowote kuanzia Sasa na kwamba hawarudi kukaa tu Bali kufanya kazi ya Siasa na kudai Katiba Mpya.

Makada hao ambao pia ni Viongozi wa ngazi za juu kabisa kwenye Chama hicho waliyasema hayo jana wakati wakizungumza na Mamia ya Wananchi na Wanachama wa Chama hicho kwenye Kongamano la 3 la vuguvugu la kudai Katiba Mpya lililofanyika Jijini Tanga ,

Awali akizungumza Moja kwa moja kwa njia ya Mtandao kutoka nchini Belgium, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu amesema kwamba iwapo patafanyika masuala ya kiufunguzi na kiusalama basi atarejea nchini.

” Tunarudi Wakati wowote kuanzia Sasa, Mimi tayari nimeshagawa Hadi Nguo za Baridi japo huku Canada kwasasa hivi Baridi imepungua Sana , Jana ( juzi) tulikuwa tunapanga na mwenzangu ni lini tuanze safari yakurudi nyumbani kwahiyo makamanda msiwe na wasiwasi tunakuja kuongeza nguvu za mapambano ya Katiba Mpya na Demokrasia kwaujumla” Alisisitiza Lema

Kwenye Kongamano hilo Wanachama wa Chama hicho na Wanachini walipata fursa yakuuliza Maswali ya moja kwa moja Viongozi hao huku lengo kubwa la Kongamano lilikuwa nikuwapatia Elimu juu ya umuhimu wakuwa na Katiba Mpya.

Makamo Mwenyekiti huyo wa Chama hicho Tundu Lissu alisema Katiba ya Sasa Haina nguvu na imetoa Mamlaka makubwa kwa Watawala waliopo Madarakani na Haina uwezo wakumuadhibu kiongozi wa ngazi za juu akiwa Madarakani au Baada ya kuondoka Madarakani,

Lissu alisema kwamba chadema ndicho chama kirakachorudisha rasimu ya katiba ya jaji Warioba hivyo majadiliano yanaendelea na serikali imeonyesha nia ya kukubali kuanza mchakato wa katiba mpya.

” Katiba ya Sasa hivi imefanyiwa marekebisho Mara 5, ukiangalia hata upatikanaji wake ulikuwa nitofauti kabisa na Nchi nyengine kama Kenya , Katiba yetu ilipatikana ndani ya Siku moja Wakati Wenzetu Kenya Katiba yao ilipatikana kwa miaka 3 , ukiangalia tofauti hizi utagundua kuwa hii ni Katiba ya Mkoloni sio ya Watanzania kwakuwa hawakuitolea maoni yao kama ilivyo Rasimu ya Warioba ” Alisisitiza Lissu

Alisema Toka Nchi ipate Uhuru Watanzania hawakuwahi kupata Fursa ya Kutoa maoni juu ya kitu wanachokita zaidi ya Rasimu ya Warioba,

” Rasimu ya Warioba ndio chombo pekee Nchini kilichopata Maoni mengi zaidi ya kimaamuzi kutoka kwa Watanzania ambapo kilipata maoni ya Watanzania Mil.3, kiukwel Nchi imetumia gharama kubwa kupata maoni hayo alafu wanakuja kuyaterekeza , nilazima tusimame imara kuhakikisha Katiba Mpya inapatikana kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025″ Alisisitiza Lissu

Aliongeza, kuwa mtu yeyote asiwaambie kuwa kudai katiba npya ni kosa siyo kosa ni haki ya kila mtanzania mtu asije akawaamisha kwamba kudai katiba mpya haifai watanzania hatujawahi kuwa na katiba ya wananchi bado tumekuwa na katiba ya watawala ambayo imeweka utaratibu wa kutoa uongozi kwa watawala hatukutoa madaraka kwa wananchi, “alisistiza Lissu.

Makamu mwenyekiti Lissu alisema kuwa hoja yake ya kwanza ni kuhusu kuwepo kwa katiba ya watawala na sio wananchi hivyo jambo hili linapaswa kupewa uzito ili kunusuru nchi.

Katika kongamano hilo Naibu katibu Mkuu bara Benson Kigaila alisema msimamo wa chama hicho ni kwamba iwapo suala la katiba mpya lisipofanyiwa kazi basi hakutakuwa na uchaguzi mkuu 2025.

“Uchaguzi hautafanyika endapo hapatakuwa na katiba mpya hatuwezi kwenda kwenye uchaguzi kufanya maigizo halafu wanapindua kura zetu, “alisisitiza Kigaila.

Alisema wao Chadema wameweka msimamo wa kwamba iwapo haitapatikana katiba mpya 2025 uchaguzi mkuu hautafanyika na kusisitiza kuwa waanze upya na waanzie kwenye rasimu ya jaji Warioba alipoishia.