November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Liberty Sparks : Jitihada zinaitajika katika utumaji na uingizaji mizigo

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

SHIRIKA lisilo la kiserikali lililojikita katika elimu na utafiti la Liberty Sparks, limesema linaimani kuwa bado jitihada zinahitajika kufanyika katika uingizaji na utumaji wa mizigo nje na ndani ya nchi.

Limeeleza jitihada hizo ni kuangalia vingezo na taratibu na muda kwasababu vikiweza kupunguza itaisaidia nchi kupaa kiuchumi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Liberty Sparks, Evans Exaud aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kikao kazi kilichokutanisha wadau wa Taasisi binafsi Kwa lengo la kujadili hatua muhimu katika juhudi za kuimarisha shughuli za kibiashara za mpakani nchini Tanzania.

Amesema wakati serikali ikilenga kufika malengo ya maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030, ni muhimu kushugulikia masuala hayo na kuweka njia kuelekea ustawi wa kiuchumi zaidi.

” Vikwazo hivi ni chagamoto kubwa Kwa wafanyabiashara wa kitanzania wanaotaka kishiriki katika biashara za kimataifa ..matokeo yake yamekuwa ni makubwa, yakizuia ukuaji wa kibiashara na kusababisha umasikini kuendelea miongoni mwa kaya,”alisema.

Alieleza kuwa utendaji wa Tanzania katika biashara za mipakani umeshidwa ikilinganishwa na baadhi ya nchi jirani kutokana na taratibu na mahitaji mbalimbali yaliowekwa kisheria Kwa biashara za mpakani ambazo zimekuwa zikiongeza muda unaohusiana na uingizaji na usafirishaji wa bidhaa.

“Mchakato wa biashara unaweza kuchukua Hadi masala 96 Kwa taratibu za mpaka vikwazo hivi ni chagamoto kubwa Kwa wafanyabiashara,”alisema.

Aliongeza kuwa
“Hii imetokana na taratibu na mahitaji mbalimbali yaliowekwa kisheria Kwa biashara za mpakani ambayo Kwa bahati mbaya yameongeza gharama na muda unaohusiana na uingizaji na usafirishaji wa bidhaa,”alisema Exaud.

Amesema Kampeni hiyo ni endelevu na imelenga zaidi kuhakikisha chagamoto ambazo zimekuwa zikisababisha watu kufanya biashara waweze kunufaika zaidi.

Alitaja baadhi ya mambo ambayo wamebaini ambayo ni Taasisi mbili kufanya kazi moja sambamba na uwepo wa taratibu ngumu.

Exaud amesema Taasisi hiyo inategemea kutoa ripoti kila baada ya miezi mitatu na kueleza kuwa dhamira ni kuchochea ushindani huru, kuwezesha uvumbuzu na ujasiriamali na hatimaye kuchangia kupunguza umasikini na kuchochea ukuaji wa kiuchumi.

Kwa upande wake mmoja wa wawakilishi kutoka Chama Cha Mawakili Tanzania (TLS), Selemani Pingoni alisema mazingira ya kibiashara katika nchi ya Tanzania yamekuwa yakiathiri taifa kupiga hatua kiuchumi pamoja na biashara ya mtu mmoja mmoja.

Amesema yapo mambo ambayo yanapaswa kufanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na serikali kutengeneza sera na kutunga Sheria na kuweka sawa miundombinu ya Barabara.

“Kazi kubwa ya serikali inapaswa kuwa Moja ya kutengeneza sera na kutunga Sheria pamoja na kuweka miundombinu na kuwaacha wafanyabiashara wafanye biashara zao,”alisema