December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

LGTI  yawakaribisha wananchi nanenane kujua kozi wanazozitoa

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

CHUO Cha Serikali za Mitaa(LGTI)-Hombolo kimewakaribishwa wananchi wanaokwenda katika maonesho ya wakulima maarufu kama nanenane kutembelea katika banda lao lilipo viwanja vya nzuguni ili kujifunza na kujua kozi zinazotolewa na  chuo hicho.

Hayo  yamesemwa jijini hapa leo Agosti 7,2024 na Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma,Tafiti na Ushauri Professa Magreth Bushesha alipotembelea  Banda la chuo hicho katika maonesho ya kitaifa ya wakulima na wafugaji Nzuguni Dodoma.

Prof.Bushesha amesema kuwa maonesho hayo ni fursa kwakila aliyekuwa anajiuliza maswali kuhusu chuo hicho na kozi zake kwani kwenye bando lao kunawataalamu ambao wataweza kuwapa majibu na kuwaelekeza vizuri.

“Tupo katika maonesho hayo kuwaonesha wananchi shughuli mbalimbali zinazofanywa na chuo cha serikali za mitaa Hombolo ,Shinyanga hususuni kozi zinazotolewa,”amesema

Ameeleza kuwa chuo hicho mwaka wa masomo 2025/26 katika Kampasi zake zote zitaanza kutoa mafunzo kwa njia ya  mtandao kwa program za cheti mastazi mpaka Digrii.

Prof.Bushesha amesema kuwa kwasasa wanatoa mafunzo hayo kwanjia ya mtandao lakini kwa ngazi ya kozi za muda mfupi mfupi.

“Tunatoa mafunzo kwanjia ya masafa kwa kozi fupi lakini kuanzia mwaka wa masomo 2025/26 tutaanza kutoa  kozi ndefu kwa njia ya masafa kwa kozi zote cheti, diploma na digrii hivyo niwakaribishe wananchi wote kuja  katika banda la chuo cha Serikali za mitaa kupata mafunzo ya ngazi zote,”amesema Prof Bushesha.

Aidha alieleza kuwa katika kozi hizo fupi wanazozitoa zimechangia kwa kiasi kikubwa kuboresha utendaji kazi kwenye sekta ya serikali za mitaa ni pamoja na mafunzo wanayoyatoa kwanjia ya fursa na vikwazo ambapo watendaji wa kata, madiwani na watendaji wote katika ngazi mbalimbali za serikali wanafundishwa namna gani wataweza  kuwaongoza wananchi kuona vikwazo vilivyopo katika maeneo yao  na kuzigeuza kuwa fursa badala ya kusubiri serikali kuja kutatua changamoto hizo

“Tumefarijika kuona watendaji wetu sasa jinsi wanavyoziangalia changamoto na kuwa fursa au namna  ya kuweza kutatua changamoto hizo moja kwa moja kabla serikali haijatia mkono wake ni jambo zuri kwa watendaji wetu sasa”, amesema Prof Bushesha .

“Sisi tunato mafunzo kwa viongozi wa serikali za mitaa ukiona watendaji wa kijiji, wenyeviti wa vijiji, madiwani, watendaji Kata wote wanapita katika chuo chetu cha serikali za mitaa ,” Amesema.

Na kuongeza” Lakini pia sio tu tumejikita kwenye viongozi wa mitaa hapana na viongozi wote katika ngazi malimbali na anyetaka kupata mafunzo ya uongozi anakaribishwa katika chuo cha serikali za mitaa,” Amesema Prof Bushesha